Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

UZINDUZI WA WARAKA WA MAPENDEKEZO YA SHERIA ILI WANAWAKE WENGI WASHIKE NAFASI ZA UONGOZI.

UZINDUZI WA WARAKA WA MAPENDEKEZO YA SHERIA ILI WANAWAKE WENGI WASHIKE NAFASI ZA UONGOZI.

Asasi za kiraia zinazotetea haki za wanawake Zanzibar kwa pamoja zitazindua waraka wa mapendekezo ya sheria ambao una lengo la kuwawezesha wanawake wengi kupata haki ya kushika nafasi za uongozi katika ngazi za maamuzi.

Uzindizi huo utafanyika siku ya Alhamis tarehe 05 Oktoba, 2023 katika ukumbi wa Bima  uliopo Madema (Mpirani ) mjini Unguja ambao utawahusisha washiriki 80 muhimu kutoka taasisi za serikali na zisizo za kiserikali pamoja   na waandishi  wa habari.

Asasi hizo ni pamoja na Chama   cha Waandishi wa Habari   Wanawake  Tanzania  Zanzibar  (TAMWA –ZNZ), Jumuiya   ya Wanasheria  Wanawake Zanzibar (ZAFELA),  Jumuiya   ya Utetezi  wa Kimazingira  na Jinsia Pemba (PEGAO) na  Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar   (JUWAUZA)

Uzinduzi huu umekuja kufuatia kukamilika kwa mchakato wa kupitia sheria, sera na katiba za vyama vya siasa ambao uliwashirikisha wadau mbali mbali na kuona  mapungufu mengi yakiwemo kutozingatiwa usawa wa kijinsia  kwa kundi la wanawake,  vijana na watu wenye ulemavu

Hali kadhalika, azimio la 1325 la Baraza la Usalama la  Umoja wa Mataifa lililotolewa tarehe 31 Oktoba mwaka  2000  linasema.  “Kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi kunakuza  demokrasia ya nchi, uchumi,  amani na utulivu kwa muda mrefu”.

Aidha, Mkataba wa kimataifa unaopinga aina zote za udhalilishaji dhidi ya wanawake, (CEDAW) wa mwaka 1979 katika kifungu cha  7 unasisitiza kuwa na haki sawa baina ya mwanamke na mwanamme katika uchaguzi na mchakato mzima wa upigaji kura  na kuchaguliwa kushika madaraka.

Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022, Zanzibar ina idadi ya watu wapatao kubwa kuliko wanaume     1,889,773 inaonyesha kuwa idadi ya wanawake ni 974,281 ambayo ni kubwa kuliko wanaume, hata hivyo, ilibainika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kuwa

jumla ya wanawake 294,237 sawa na asilimia 51 waliandikishwa kama wapiga kura ikilinganishwa na wanaume 272,115 ambao ni sawa na asilimia 49.Imetolewa na ZAFELA, PEGAO, TAMWA-ZNZ na JUWAUZA
*****************************************************************************************************************************************************

Press Statement

LAUNCHING OF A POSITION PAPER – STRENGTHENING WOMEN’S PARTICIPATION IN LEADERSHIP

Civil society organizations advocating for women’s rights in Zanzibar are expected to launch a position paper aimed at empowering women to seek leadership positions at decision-making levels. The launch is scheduled to take place on Thursday, 5th October,  2023, at the Bima Hall (Mpirani) near Madema , Unguja, and will involve 80 plus key stakeholders from the government, non-governmental organizations, and members of the media.

These organizations include the Tanzania Media Women’s Association, Zanzibar (TAMWA-ZNZ), Zanzibar Female Lawyers Association (ZAFELA), Pemba Environmental and Gender Advocacy Organization (PEGAO), and Zanzibar Disabled Women’s Association (JUWAUZA).

The launch follows the completion of a process that reviewed laws, policies, and party constitutions, involving various stakeholders, which identified many shortcomings, including the lack of gender equality consideration for young women and persons with disabilities.

Furthermore, United Nations Security Council Resolution 1325 issued on October 31, 2000, states, “Increasing women’s participation at decision-making levels that promotes the long-term democracy, economy, peace, and stability of a country.”

Additionally, the Convention on the Elimination of All Forms of Discrimination against Women (CEDAW) of 1979, in Article 7, emphasizes equal rights between women and men in the electoral process and the entire process of voting and being elected to leadership positions.

According to 2022 Population and Housing Census, Zanzibar population is approximately 1,889,773, shows that the number of women exceeds that of men, with 974,281 women compared to men. However, in the 2020 General Election, it was revealed that a total of 294,237 women, equivalent to 51%, were registered as voters, compared to 272,115 men, which is 49%.Issued by ZAFELA, PEGAO, TAMWA-ZNZ, and JUWAUZA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00