Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

Kazi 529 zapokelewa kuwania tuzo za umahiri za uandishi wa habari za takwimu za wanawake na uongozi.

Kazi 529 zapokelewa kuwania tuzo za umahiri za uandishi wa habari za takwimu za wanawake na uongozi.

JUMLA ya kazi 529 za waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari zimewasilishwa kwa ajili ya kuwania tuzo za umahiri za uandishi wa habari za takwimu za wanawake na uongozi.

Miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na vipindi vya redio, televisheni, makala za magazeti na zile kutoka katika mitandao ya kijamii zilizoandikwa na kurushwa katika vyombo vyao kuanzia mwezi Janauari hadi Disemba 31, 2023.

Kazi hizo zinaonesha ni jinsi gani waandishi wamekuza mwamko wa kuandika habari za uongozi kwa wanawake ambapo zinashajihisha wanawake na vijana wakike kujiamini zaidi na kuwa na matumaini ya kupata nafasi mbali mbali za uongozi lakini pia zinaielimisha jamii kuhusu umuhimu wa wanawake katika uongozi.

Lengo la tuzo hizo ni kuhimiza waandishi wa habari kutumia kalamu zao na vyombo vya habari kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa masuala ya wanawake katika uongozi na hivyo kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi mbalimbali za maamuzi.

Hii ni mara ya tatu kwa tunzo hizo kufanyika hapa Zanzibar na kwa mwaka huu zinatarajiwa kufanyika mapema mwezi Machi, 2024.

Tuzo za umahiri za uandishi wa habari za takwimu za wanawake na uongozi zinaandaliwa kwa pamoja na  Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar, (TAMWA – ZNZ),  Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Jumuiya inayojihusisha na Mazingira, Usawa wa Kijinsia, na Utetezi Pemba (PEGAO), kwa kushirikiana na Ubalozi wa Norway nchini Tanzania.

Dkt. Mzuri Issa,
Mkurugenzi,
TAMWA ZNZ.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00