Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

“Wanawake wenye nia ya kugombea nafasi ya uongozi kuepuka unyanyasaji mitandaoni”

“Wanawake wenye nia ya kugombea nafasi ya uongozi kuepuka unyanyasaji mitandaoni”

Wanawake wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi nchini wametakiwa kujitokeza kugombea nafasi za uongozi na kuepuka vikwazo vinavyyowekwa na baadhi ya watu wenye nia ya kurudisha nyuma ushiriki wa wanawake wa kufikia lengo la usawa wa 50 kwa 50 katika uongozi.

Mkurugenzi TAMWA-ZNZ Dkt. Mzuri Issa ameyasema hayo katika mkutano na wadau wa masuala ya wanawake na uongozi kujadili unyanyasaji wa wanawake mitandaoni huko huko ofisi ya TAMWA-ZNZ Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

Dkt. Mzuri alieleza kuwa, wakati umefika kwa wanawake kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kwa kujiamini na kushinda changamoto hizo kwani wadau mbali mbali wanachukua jitihada kuhakikisha usawa wa kijinsia katika uongozi unasimamiwa na kufanya kazi ipasavyo.

‘’Kwa sasa tumepata fursa nyengine ya kuwanyanyua wanawake na kuwawekea mazingira mazuri ili waweze kujiona wako salama wanaposhiriki katika nafasi za uongozi na kufikia usawa wa 50 kwa 50″, alieleza Dkt. Mzuri Issa, Mkurugenzi TAMWA-ZNZ.

Akiwasilisha mada kuhusu rushwa ya ngono katika mkutano huo Afisa elimu Taasisi ya Kupambambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) Yussuf Juma Suleiman amesema katiba ya Zanzibar pamoja na mikataba ya kimataifa imetoa nafasi sawa kwa wanawake na wanaume kushiriki katika uongozi hivyo ni vyema kila mmoja kuchukuwa hatua kuhakikisha usawa katika nafasi za uongozi unapatikana.

” Kutungwa kwa sheria za kimataifa pamoja na mikataba mbalimbali ukiwemo mkataba wa Afrika wa haki za wanawake na watoto na mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake, ni moja wapo ya mifano michache ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia (rushwa ya ngono)’’ Yussuf Juma Suleiman, Afisa elimu kutoka ZAECA.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa Zanzibar Abdulrazak S. Ali amesema awali wanawake walipitia changamoto nyingi katika kugombania nafasi za uongozi zikiwemo uchumi mdogo, mfumo wa uteuzi ndani ya vyama vya siasa, ubaguzi, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia pamoja na kukosa nafasi katika vyombo vya maamuzi ambapo kwa sasa changamoto hizo zimepatiwa ufumbuzi.

“Mwaka 2024 kumefanyika marekebisho makubwa ambayo yatapelekea fursa zaidi kwa wanawake kuweza kupata nafasi mbali mbali ndani ya vyama vya siasa, maboresho hayo yamezingatia jinsia na ujumuishi, kuongezwa kwa kifungu cha 10 C ndani ya marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2024 ambayo yatasaidia uwajibika kwa vyama vya siasa kuwa na sera ya jinsia kwa muda wote’’ ameeleza Abdulrazak S. Ali.

Kwa upande mwengine amewataka wanawake kuweka imani kwa Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kwani iko mstari wa mbele kuhakikisha usawa wa jinsia unapatikana katika vyama vya siasa. 

” Tuwe na imani na Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kwani tayari imeanzisha dawati la jinsia na kupokea kesi za masuala yanayohusiana na jinsia bila ya upendeleo na kuzipatia ufumbuzi”, amesisitiza Abdulrazak S. Ali.

Akifunga mkutano huo Mjumbe wa Bodi TAMWA-ZNZ Hawra Shamte, amewaomba wadau kuelimisha jamii umuhimu wa wanawake kugombea nafasi za uongozi sambamba kukomesha vitendo vya unyanyasaji mtandaoni na rushwa ya ngono dhidi ya wanawake.

Mkutano huo wa siku moja umewashirikisha wadau kutoka taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, waandishi wa habari na wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari kujadili masuala ya wanawake na uongozi ikiwemo unyanyasaji wa wanawake mitandaoni.

MWISHO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00