Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike duniani, wadau wa michezo kwamaendeleo Zanzibar ambao ni Jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar (ZAFELA),Kituo cha mijadala kwa vijana (CYD) na Chama cha Waandishi wa Habari WanawakeTanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani(GIZ) imeandaa shughuli mbalimbali za michezo kwa maendeleo (S4D) zenye lengo lakuhamasisha usawa wa kijinsia katika michezo.Maadhimisho hayo yatashirikisha wanafunzi kutoka skuli za Unguja (wilaya za Kaskazinina Mjini Unguja) na yataanza kwa shamrashamra za mechi za Mpira wa pete (Netball) zakirafiki, zitakazohusisha timu za watoto wa kike kutoka skuli za Tumbatu, Jongowe,Mkokotoni, Mto wa Pwani, Kianga, Mtoni, Kiembe Samaki “B” na Uroa.Shughuli nyengine zitakazofanyika ni kufanya ziara kwenye skuli mbalimbali nakuendesha michezo kwa maendeleo (S4D) ambayo itawafundisha wanafunzi namna yakujikinga dhidi ya ukatili wa kijinsia, pamoja na kuwaelimisha kuhusu masuala yawanawake na uongozi. Wanafunzi pia watashiriki kwenye uchoraji wa picha ambazozitaakisi maudhui ya S4D na kuwapa fursa ya kuelezea mawazo yao kuhusu michezo nausawa wa kijinsia.Kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika siku ya Jumamosi tarehe 12 Oktoba, 2024ambapo itachezwa mechi ya fainali ya Mpira wa pete (Netball) na pia picha zilizochorwana wanafunzi zitaoneshwa. Mgeni rasmi ambae ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya JamiiJinsia, Wazee na Watoto Mhe. Anna Atanas Paul ataongoza shughuli ya kukabidhi zawadikwa washiriki wote, ikiwa ni pamoja na vikombe, medali, na vifaa vya michezo.Maadhimisho hayo ni sehemu ya mkakati wa wadau wa S4D Zanzibar wa kuendeleza nakuhamasisha ushiriki wa watoto wa kike kwenye michezo huku wakipinga ukatili wakijinsia na kuboresha usawa wa kijinsia hapa visiwani.
- Phone: +255 772 378 378
- Mon-Fri (8am - 4pm)
- info@tamwaznz.or.tz
Edit Content
About Us
TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.
Contact Info
- TUNGUU ZAZNZIBAR TANZANIA, P.O.BOX 741
- +255 772 378 378 +255 714543132
- info@tamwaznz.or.tz
- Week Days: 08.00 to 16.00