Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi Wahabari Wanawake Tanzania, TAMWA ZNZ, Dkt Mzuri Issa amewataka waandishi wahabari kuvitumia vyombo vya habari ipasavyo katika kuibuwa changamoto zinazoikabili jamii.

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi Wahabari Wanawake Tanzania, TAMWA ZNZ, Dkt Mzuri Issa amewataka waandishi wahabari kuvitumia vyombo vya habari ipasavyo katika kuibuwa changamoto zinazoikabili jamii.
Akifunguwa mkutano wa siku moja katika maadhimisho ya siku ya Radio Duniani, yaliyofanyika TAMWA Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja amesema wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo athari za mabadiliko ya tabianchi, uongozi katika vyama vya siasa na ukatili wa kijinsia ambazo huwarudisha nyuma kimaendeleo na kuwafanya wawe duni.
Dkt Mzuri amesema kwa ushirikiano mkubwa na vyombo vya habari TAMWA ZNZ imefanikiwa kutoa jumla ya habari 778 kwa mwaka 2024 kupitia program mbali mbali na vyombo tofauti vya habari , kati ya hizo habari 502 zilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii, 120 kwenye magazeti, 101 kwenye radio na 55 kwenye Televisheni.
Aidha Dkt Mzuri katika maadhimisho hayo amesisitiza kupatikana kwa Sheria mpya ya Habari itakayoleta mageuzi kwa waandishi na jamii kiujumla na kutoa fursa ya kutumia haki yao ya Kikatiba kwa kutoa maoni yao katika jambo husika kwa maslahi ya umma.
“Sheria ya habari bado inalalamikiwa kwa kuminya ulinzi kwa Waandishi na hata jamii na kutoa uhuru kwa viongozi, tunataka mabadilko ya sheria hii,” Dkt Mzuri.
Nae Mjumbe wa bodi TAMWA ZNZ Haura Shamte amesema redio zinakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo nyenzo za kufanyia kazi hasa katika ulimwengu huu wa Sayansi na Teknologia, kukosa wafanyakazi wenye weledi wanaosababisha mporomoko wa maadili kwa kurusha maudhui yanayokiuka mila, silka na utamaduni wa Kizanzibari.
Washiriki wa mkutano huo wamewaomba wamiliki wa vyombo vya habari kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara waandishi wahabari ambayo yatasaidia kuongeza ubunifu wa kutengeneza maudhui yanayokubalika katika jamii.
Siku ya kimataifa ya redio huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 13 Febuari ili kuthamini mchango wa redio katika jamii, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu huu ni “Redio na mabadiliko ya tabianch”i.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00