
Leo tarehe 13 Febuari 2025 TAMWA Zanzibar imepokea Ugeni wa wadau wa maendeleo wa kimataifa kutoka taasisi mbalimbali na kufanya mazungumzo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na TAMWA ZNZ zikiwemo kumnyanyua mwanamke katika masula ya uongozi, kiuchumi, kisiasa na kupinga ukatili wa kijinsia. Ugeni huo uliongozwa na Wizara ya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Zanzibar na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.