Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

ZAMECO Yalaani Hatua za Kudhibiti Vyombo vya Habari, Yatetea Haki yaKupata Taarifa Kipindi cha Uchaguzi.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE: 25/10/2025
ZAMECO Yalaani Hatua za Kudhibiti Vyombo vya Habari, Yatetea Haki ya
Kupata Taarifa Kipindi cha Uchaguzi.
Kamati ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar (ZAMECO) inasikitishwa na hatua
ya Tume ya Utangazaji ya Zanzibar kutoa taarifa inayoweka orodha ya Vyombo vya Habari
vya Mtadaoni inavyovitaja kuwa vinafanya kazi kinyume cha sheria ambayo Tume hiyo
inaisimamia na kutishia kuvichukulia hatua kali za kisheria iliyoitoa tarehe 20 Mwezi
Oktoba 2025 na nyakati nyengine tofauti.
ZAMECO ambayo ni Kamati inayojumuisha watendaji wabobezi wa sekta ya Habari na
utetezi wa haki za binadamu kutoka asasi mbambali za kiraia zilizopo Zanzibar,
tunalichukulia tamko hilo kuwa ni hatua inayoweza kudhoofisha jitihada za sekta binafsi
kukuza uhuru wa kujieleza na kuimarisha upatikanaji wa taarifa huru nchini.
Wakati Zanzibar kama sehemu ya dunia inajitahidi kwenda na wakati, kutoa mawazo
mbadala na mifumo ya kisasa ya mawasiliano ya kiteknolojia (Social Media), hatua hii ya
Tume inaonesha kurudisha nyuma jitihada hizi.
Vyombo vilivyotajwa katika taarifa hiyo ni pamoja na TIFU ONLINE TV, MARHABA
ONLINE TV, VUGA ONLINE TV, BUSATI ONLINE TV, KASUSI ONLINE TV,
DIGITAL ONLINE TV, DIGITAL ONLINE TV, LEADERS ONLINE TV, ZANZIBAR
YETU ONLINE TV, MAWENGI ONLINE TV, JIMBI ONLINE TV NA MU ONLINE TV.
Kuwepo kwa mitandao hiyo ya habari kunawafanya pia vijana waweze kujiajiri na kupata
kipato chochote kwa maisha yao na wengine kufanyia kazi mafunzo yao waliyosomeshwa
vyuoni wakati wakisubiria ajira za kudumu.
Ikumbukwe kuwa haki ya kupata taarifa ni ya kikatiba kama inavyoelezwa kwenye Katiba
ya Zanzibar ya Mwaka 1984 (Toleo la 2010 katika Ibara ya 18 – pamoja na Mikataba ya
Kimataifa ikiwemo Azimio la Ulimwengu la Haki za Binaadam (UDHR, 1948); Ibara ya 19,
Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR, 1966); Ibara ya 19(2) na
Mkataba wa Afrika wa Haki za Binaadam na Watu (ACHPR, 1981) kupitia Ibara ya 9.
Hivyo, kitendo cha Tume kuvitaja vyombo hivyo hadharani bila ya kuhusisha “majadiliano
jumuishi” na wadau inaleta taswira ya kuzuia uhuru wa kujieleza na haki ya watu kupata
taarifa hasa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
Katika mustakbali wa kujenga demokrasia iliyo madhubuti, kazi ya Tume ya Utangazaji
ni kusaidia na kuinua vyombo vya habari ikiwemo kujua maendeleo na changamoto zao
na kuweza kuwatatulia na kwamba jambo la kuwafungia linapaswa kuwa la mwisho
baada ya kufuatwa utaratibu mzuri wa ushirikishi na uwazi.
Katika kufuatilia kwake kwa baadhi ya vyombo hivi, ZAMECO imegundua kuwa kuna
vyombo vimepata changamoto za kifedha na baadhi yake vimehusishwa na makosa ya
kimaudhui ambayo hayajaweza kubainishwa ipasavyo.
Mfano, Sheria ya Wakala wa Maendeleo na Uanuwai wa Vyombo vya Habari ya mwaka
2022 (Media Development and Diversity Agency Act, 2002) ya Afrika ya Kusini imeweka
mfumo mzuri wa kusaidia vyombo vya Habari, katika kifungu cha 17 cha sheria hii
kimeeleza aina za msaada ambazo inaweza kutoa:

  1. Msaada wa kifedha, kama vile ruzuku za moja kwa moja au fedha za dharura
    zinazolenga kuimarisha au kuokoa vyombo vya habari vinavyokabiliwa na
    changamoto za kifedha;
  2. Mafunzo na ujenzi wa uwezo katika nyanja za uzalishaji na usambazaji wa
    maudhui ya habari;
  3. Msaada usio wa moja kwa moja, kwa mfano kupitia mashirika ya umma au
    taasisi za kifedha, kwa kupata punguzo la bei au viwango vya chini vya huduma
    kama vile matangazo, usambazaji wa matangazo ya redio/televisheni, barua, na
    huduma za simu.
    Ni wito wetu kwamba Tume ya Utangazaji itoe ushirikiano na wamiliki wa vyombo hivi
    vya habari na Wadau wa Habari, badala ya kutumia mbinu ya vikwazo ili kuweka
    mazingira rafiki kwa vyombo vya habari kufanya kazi kwa mujibu wa sheria lakini bila ya
    kuathiri uhuru wa habari. Ni muhimu kuzingatia kuwa katika kipindi cha kuelekea
    uchaguzi mkuu, kila sauti na jukwaa la habari lina nafasi kubwa katika kukuza amani,
    mshikamano na maamuzi yenye ufahamu miongoni mwa wananchi.
    Tume ya Utangazaji ikumbuke kuwa kazi ya Uandishi wa habari ni ya kitaaluma na
    ambayo inapaswa kufuata misingi yake na kujiendesha wenyewe na kwamba vyombo
    vya sheria ndivyo kimsingi vinapaswa kushughulika na ambao watakwenda kinyume na
    taaluma hiyo ya habari.
    Sambamba na hilo, ZAMECO inasikitishwa na taarifa inazopokea kwa Waandishi wa
    Habari hasa vijana za kunyimwa mashirikiano na watendaji wa Serikali katika kupata
    taarifa katika ngazi zote kama kwamba katika kipindi hichi masuala mengine yeyote
    yasiendelee. Hii inakatisha tamaa jitihada za waandishi hawa wa habari ambao wana
    azma ya kujenga ustawi na haki za makundi mbali mbali katika jamii na kuonesha
    kutokuwajibika kwa watendaji.
    Wakati huohuo, ZAMECO inapongeza kipindi cha PAMBAZUKO kinachorushwa na
    Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC Redio) kwa kuwa jukwaa muhimu la kuwapa nafasi
    Wananchi ya kueleza matatizo yanayoathiri maisha yao ya kila siku hususan kwenye eneo
    la huduma za kijamii. Kupitia jukwaa hilo, Wananchi hutuma maelezo ya ujumbe mfupi
    (SMS) na kusomwa hewani. Kinachofurahisha zaidi ni hatua wanayochukuwa waandaaji
    kipindi ya kuwasiliana na watendaji wa Serikali na kuyaeleza matatizo hivyo kushawishi
    utatuzi na majibu kutolewa katika muda mfupi.
    Ni aina ya vipindi vinavyohitajika sana kwa kuwa vinashawishi uwajibikaji wa mamlaka za
    kiserikali. Na huu ndio mfano bora wa uandishi wa habari unaohimizwa kwa vile
    unachochea uwajibikaji, ushirikishwaji na kuchagiza maendeleo ya jamii.
    ZAMECO inaendelea kusimama kidete kutetea uhuru wa habari, Uwazi, na Upatikanaji wa
    Taarifa, ikiamini kuwa jamii inayopata habari sahihi na kwa wakati ni jamii yenye nguvu,
    amani, na inayojua wajibu wake katika kulinda demokrasia na maendeleo endelevu katika
    nchi.
    IMETOLEWA NA:
    Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC),
    Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA-ZNZ)
    Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA)
    Baraza la Habari Tanzania, Zanzibar (MCT, ZNZ)
    Jukwaa la Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Zanzibar (THRDC, ZNZ).

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00