Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

TAMWA ZANZIBAR YATOA WITO WA ULINZI WA WATOTO KIPINDI CHA SIKUKUU YA EID EL-FITRI

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE
T ANZANIA
P. O. Box 741 Tunguu Zanzibar, TEL: 0242232263
Mobile No. 0777479858

Email: info@tamwaznz.or.tz

19/03/2026.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
TAMWA ZANZIBAR YATOA WITO WA ULINZI WA WATOTO
KIPINDI CHA SIKUKUU YA EID EL-FITRI
Wakati tukielekea katika sherehe ya Sikukuu ya Eid-El-Fitri, Chama cha Waandishi wa
Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA – ZNZ) kinatoa wito kwa wazazi,
walezi na jamii kuchukua tahadhari za makusudi katika kulinda usalama na ustawi wa
watoto kipindi chote cha sikukuu.
Kipindi cha sikukuu huambatana na mikusanyiko na shughuli mbalimbali za kijamii
ambazo bila uangalizi wa karibu, zinaweza kuwaweka watoto katika hatari ya vitendo
vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia.
Karibu kila mwaka wakati wa sherehe za Sikukuu ya Eid El Fitri au Eid El Adh-ha
huripotiwa matukio ya udhalilishaji kwa watoto katika maeneo mbali mbali ya
Zanzibar, ikiwemo kupotea kwa watoto, kubakwa, kulawitiwa, kutoroshwa na
matukio ya mengine ya aina hiyo.
Takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
kwa mwezi Januari 2026 zinaonesha ongezeko la vitendo vya udhalilishaji, katika
kipindi hicho, jumla ya matukio 113 yaliripotiwa, ambapo matukio 91, sawa na
asilimia 80.5, yaliwahusu watoto, ukilinganisha na mwezi Januari 2025, ambapo
jumla ya matukio 103 yaliripotiwa na kati yake matukio 87 (asilimia 84.5) yalihusisha
watoto.
Takwimu hizi zinaashiria kuwa vitendo vya udhalilishaji vimeshamiri na kutokana na
uzoefu wa miaka ya nyuma huongezeka zaidi wakati huu wa sikukuu kutokana na
watoto kuachiwa kutembea huru kwa wakati mrefu nje na ndani ya viwanja vya
kusherehekea.
TAMWA – ZNZ inasisitiza kuwa ni jukumu la pamoja kuhakikisha watoto hawatoki
peke yao kwenda sikukuuni, hivyo wazazi na walezi wanahimizwa kuwasimamia
watoto wao kwa karibu, kuongozana nao na kuhakikisha wanawanarejea nyumbani
salama.
Aidha, ni muhimu kuepuka kuwapa watoto jukumu la kuwasimamia au kuwaongoza
watoto wenzao, kwani nao bado wanahitaji uangalizi na ulinzi wa watu wazima,
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tz
pamoja kufuatilia mienendo isiyo ya kawaida na kutoa taarifa mapema kwa mamlaka
husika.
TAMWA -ZNZ inaliomba pia Jeshi la Polisi nchini kuimarisha ulinzi katika kipindi hichi
chote pamoja na matangazo ili kuwalinda watoto ambao wako kwenye kundi la hatari
kutekwa na kubakwa.
Hivyo, TAMWA – Zanzibar inatoa wito kwa wazazi kuzungumza na watoto wao
kuhusu usalama wao, kuwajengea ujasiri wa kuripoti matukio yoyote ya vitisho au
unyanyasaji, na kuhakikisha wanakuwa katika uangalizi wa watu wanaoaminika
wakati wote.
Vitendo ya udhalilishaji vinazuilika endapo jamii itakuwa tayari kuelimishana na
kukatazana maovu kwani mhalifu hatoki mbali, bali hutoka ndani ya familia, majirani
pamoja na jamii, hivyo kila mmoja atimize wajibu wake katika kukataa udhalilishaji
kwa wanawake na watoto na kuhakikisha sikukuu ya Eid el-Fitri inakuwa ya furaha,
amani na usalama kwa wote.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari
TAMWA Zanzibar
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tz

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00