Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

WAOMBAJI WA RUZUKU 734 WAWASILISHA MAOMBI KATIKA MRADI WA VIUNGO ZANZIBAR.

WAOMBAJI WA RUZUKU 734 WAWASILISHA MAOMBI KATIKA MRADI WA VIUNGO ZANZIBAR.

Jumla ya waombaji 734 wamefanikiwa kujaza na kuzirudisha fomu za maombi ya ruzuku ya  mradi wa VIUNGO ambao  umelenga kutoa rukuzu kwa wanufaika wake waliosajiliwa katika visiwa vya  Unguja na Pemba.

Utoaji wa ruzuku hiyo ni moja ya malengo ya mradi wa VIUNGO kwa ajili ya kuwawezesha  wanufaika wa mradi huo katika  kukuza  kilimo cha mboga, matunda na viungo  na kuongeza thamani ya mazao hayo ili kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla .

Kufuatia kupokelewa kwa maombi hayo kutoka kwa wakulima, wachakataji na wadau wa mnyororo wa thamani kwa mazao ya kilimo kutoka Unguja na Pemba, ambapo mradi wa VIUNGO umeunda kamati ya wajumbe nane (8) yenye jukumu la kupitia ,na kuhakiki maombi  ya ruzuku za wanufaika hao ili kupewa ruzuku hiyo.

Kamati hiyo  imeundwa na wajumbe kutoka Wizara ya kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo na  Wizara ya fedha na Mpango Zanzibar Pamoja na watendaji wa mradi huo.

Katika kuhakikisha maombi hayo yanakidhi vigezo vilivyowekwa na mradi ,kamati hiyo itakaa kwa muda wa wiki moja kwa lengo la kuzipitia na kuhakiki maombi yote.

Jumla ya wanufaika wa mradi wa VIUNGO 70 kati ya 734 waliiomba watapata ruzuku ambayo itachochea ufikiaji wa malengo ya kukuza mnyororo wa thamani kwa mazao ya viungo, mboga na matunda na kuinua kilimo cha wakulima wadogo wadogo Zanzibar.

Value Web Horticulture and Income Growth Project unajulikana kama mradi wa VIUNGO, ni mradi wa miaka minne umeanza Juni 2020 hadi Juni 2024, upo chini ya program ya AGRI-CONNECT na unatekelezwa Unguja na Pemba na Jumuiya ya PDF wakishirikiana na Community Forest Pemba (CFP) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar (TAMWA-ZNZ) kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

Imetolewa na Kitengo cha Habari na mawasiliano

TAMWA, Zanzibar 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00