Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

TAMWA ZNZ yaitaka jamii kuwalinda watoto dhidi ya udhalilishaji

TAMWA ZNZ yaitaka jamii kuwalinda watoto dhidi ya udhalilishaji

Wazee wanashauriwa kuchukua hadhari kubwa katika kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya udhalilishaji katika kipindi hichi cha likizo ya mwezi Disemba inayoambatana na sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.

Kwa mujibu wa ripoti ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar, inaonesha kuwa ndani ya mwezi wa Novemba mwaka huu matukio 172 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa ambapo waathirika 147 walikua ni watoto sawa na asilimia 85.4.

Ripoti hiyo pia inaonesha muda wa matukio hayo zaidi ni kuanzia saa 9 mchana hadi saa 3 usiku, kipindi ambacho baadhi ya watoto wanakuwa nje kwa kucheza ama wanakuwa matembezini na watoto wenzao.

Takwimu za udhalilishaji wa kijinsia zinaonesha kuwa matukeo mengi hutokea wakati wa sikukuu hivyo ni vyema jamii kujipanga ili kubadilisha hali hiyo na hivyo kuwalinda watoto dhidi ya vitendo hivi viovu.

Kutokana na hali hiyo, jamiii inahitaji kuwa makini kuwafahamisha watoto juu ya kuwepo kwa watu waovu na pia kuchukua hadhari kwa watoto wao ili kuwalinda na kupunguza kasi za kuongezeka kwa vitendo hivyo dhidi yao.

Watoto na wazee kwa pamoja wanaweza kuchukua mbinu za ulinzi pamoja na kuelewa viashiria hatarishi ili kuvibaini na kuvichukulia hatua kabla ya tukio lenyewe.

Wakati huo huo tunaendelea kuviomba vyombo vya sheria kuharakisha kufanya upelelezi na upatikanaji wa haki ili kuwatisha watu ambao wana tabia hii na wanaotaka kufanya matendo hayo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Mtakwimu ni tukio moja tu kati ya matukio 172 sawa na asilimia 0.6 ndilo lililofikishwa mahakamani, hali inayoonesha kuwa bado masuala ya upelelezi yanachukua muda mrefu na hivyo kuhatarisha upatikanaji wa haki.

Vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa watoto vina athari kubwa kwa watoto ikiwemo kisaikolojia, kiakili na  kimwili na kuvunja ndoto za watoto za kimaendeleo pamoja na kuondosha wito maarufu wa kinchi na wakidunia kwamba asiachwe nyuma mtu yeyote.

Dkt. Mzuri Issa,

Mkurugenzi,    

TAMWA ZNZ.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00