Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

TAMWA ZNZ yaomba kupungua kwa malalamiko ya udhalilishaji

TAMWA ZNZ yaomba kupungua kwa malalamiko ya udhalilishaji

Jamii inahitaji kutafuta mbinu za kupambana na vitendo vya udhalilishaji ambavyo vinaripotiwa kuongezeka kiasi cha kuwa na matukio zaidi ya 150 kwa mwezi mmoja tu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar, inaonesha kuwa ndani ya mwezi Octoba matukio yalikuwa ni 199 na mwezi wa Novemba jumla ya matukio 172 yameripotiwa, na katika matukio yote haya waathirika wakubwa wa vitendo hivi ni wanawake na watoto.

Ikilinganishwa na idadi ya matukio ya mwaka 2022 ambapo jumla ya matukio 1361 yaliripotiwa, idadi hiyo inaweza kuongezeka kupita kiasi kutokana na idadi kubwa inayoripotiwa kwa kila mwezi ndani ya mwaka 2023.

Ongezeko hili linahitaji kuangaliwa katika pande kuu mbili ambazo ni vyombo vya kisheria pamoja na jamii kwamba kwa kiasi gani sehemu hizo zinachukua jukumu lake ipasavyo.

Kwa mfano upande wa vyombo vya sheria vihakikishe haki inapatikana kwa watu wote kama inavyostahiki na kwamba wahalifu wote bila ya ubaguzi walipie makosa yao. Pia sheria zinahitaji ziwe vizuri, zinatekelezeka ipasavyo na kwamba Maafisa wa vyombo vya sheria wanashughulikiwa ipasavyo pale wanapokengeuka majukumu yao.

Jamii kwa upande wake inapaswa kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na kutoa elimu kwa watu walioko katika makundi hatarishi ili wasifanye vitendo vya kudhalilisha wengine, kuwalinda watoto dhidi ya udhalilishaji na kutoa ushahidi pale inapohitajika.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Mtakwimu kwa mwezi wa Novemba kati ya matukio 172 ni tukio moja tu ndilo lililofikishwa mahakamani hali ambayo inahitaji kuangaliwa vizuri. 

Changamoto nyengine ni juu ya ukosefu wa utumiaji mzuri wa sheria kwa mfano sheria ya ushahidi No. 9 ya mwaka 2016 imetoa fursa ya kutumia ushahidi wa kielektroniki lakini bado hautumiki ipaswavyo na hivyo kuhatarisha kupotea kwa mafaili na kuleta usumbufu kwa watoa ushahidi hasa watoto na watu wenye ulemavu.

Hivyo, tunatoa wito kwa vyombo vya sheria kuzidisha kasi ya upelelelezi na kuwekeza katika teknolojia kwa ajili ya kusikiliza malalamiko na kuwapa unafuuu watoto wadogo.

TAMWA ZNZ pia inaendelea kutoa wito kwa vijana kujipangia mipango madhubuti ya kutokuingia katika vitendo hivi ikiwemo kuacha kufuata vishawishi, kutokuendekeza mihemuko na pia kujidhibiti dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao.

Dkt. Mzuri Issa,

Mkurugenzi,      

TAMWA ZNZ.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00