Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

NED yaitembelea TAMWA ZNZ

Ujumbe kutoka shirika la National Endowment for Democracy (NED), ambao ni washirika wa maendeleo wa TAMWA ZNZ kupitia programu ya kuwaendeleza waandishi wa habari vijana kuandika habari za wanawake na uongozi (YMF), wametembelea ofisi za TAMWA ZNZ pamoja na vyombo vya habari ikiwemo Shirika la Magazeti ya Serikali na Redio Jamii KATI fm kwa ajili ya kuzungumzia na kuona maendeleo ya vijana hao, vyombo vya habari na masuala ya wanawake na uongozi kwa ujumla.

Akizungumza katika mkutano uliowashirikisha watendaji kutoka (NED), waandishi wa habari vijana, wakurugenzi wa redio na wahariri wa vyombo vya habari, Dkt Mzuri amesema kuna mambo kadhaa yanayowakwaza wanawake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Dk Mzuri amesema TAMWA ZNZ kushirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo wamekuwa wakitoa mafunzo mbalimbali kwa waandishi wa habari hao ili kuwaongezea zaidi ujuzi waweze kuandika habari za wanawake na uongozi, pamoja na kuondosha mitazamo hasi katika jamii. 

“Tunaelekea katika kipindi cha uchaguzi mkuu 2025 hivyo waandishi wa habari tunawategemea katika upande huu kuandika zaidi na kufanya vipindi vingi ili tuone kasi ya wanawake inakuwa kubwa katika kugombea  ngazi mbalimbali  majimboni,” Dk Mzuri.

Nae meneja wa programu kutoka NED, Mary Kagunyi amesema wamefarajika na jitihada mbali mbali zinazofanywa na TAMWA ZNZ katika kushawishi jamii kuondokana na mitazamo hasi, hususan kuhusu wanawake kugombea nafasi za Uongozi.

“Tumefarajika na kazi kubwa inayofanywa na TAMWA ZNZ katika kuongeza nguvu na kuifahamisha jamii kujuwa haki zao pamoja na kugombea nafasi za Uongozi kuanzia katika ngazi ya familia hadi Taifa,” Mary Kagunyi.

Mradi wa kuwawezesha waandishi wa habari vijana (YMF) kuandika habari za wanawake na uongozi umewashirikisha waandishi vijana ishirini na wanne (24) kutoka Unguja na Pemba ambao unatekelezwa na  TAMWA ZNZ kwa kushirikiana  na shirika la National Endowment for Democracy (NED).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00