TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Vikundi 42 vya Watu Wenye Ulemavu Vyajiimarisha kiuchumi Kupitia
iSAVE KIJALUBA
Wanachama Wanufaika na Mafunzo na Mikopo
Jumla ya shilingi milioni 143,077,862 zimekusanywa katika mzunguko wa kwanza
wa mwaka mmoja kwa vikundi 42 vya kuweka na kukopa vya iSAVE KIJALUBA
kutoka katika Wilaya ya Kusini Unguja na Wilaya ya Chakechake Pemba ambapo
fedha hizi zinajumuisha hisa zilizowekwa, pesa za mfuko wa jamii na faida kutoka
katika ada ya usimamizi ya uchukuaji wa mikopo.
Vikundi hivyo vina jumla wanachama 1,186 wakiwemo watu wenye ulemavu 811
ambao ni sawa na asilimia 68 ya wanachama wote ambapo kati ya hao 811
wanawake ni 422 na wanaume ni 389.
Katika kipindi cha mwaka mmoja vikundi hivi vimepatiwa elimu mbalimbali
ikiwemo elimu ya kuendesha biashara, elimu ya kuweka akiba na kukopa pia
utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo sabuni, achari, ushonaji wa mikoba
ya ukili na hata ukulima wa mbogamboga, ambapo biashara hizi kwa kiasi
kikubwa zimewasaidia kujikomboa kiuchumi na wanaziendesha kwa kupitia
mikopo ambayo wanaichukua ndani ya vikundi vyao.
Wanavikundi wa iSAVE KIJALUBA wanajivunia vikundi hivyo kwa kuwa
vimewapa muamko wa kujitegemea na kuwasaidia katika shughuli mbalimbali
ikiwemo kusomesha watoto wao, kuendeleza biashara, mahitaji ya nyumbani na
mengineyo, pia kuweko kwa mfuko wa jamii umewasaidia katika maafa, misiba na
mambo mengine ya kijamii.“Kikundi hichi kinatusadia sana na tunajivunia khasa, tunafanya biashara,
tunakopa na maisha yamebadilika sivo kama yalivyokuwa, tunashukuru sana kwa
kuanzishiwa vikundi hivi”, anasema Asha Amour mwanakikundi cha “nyota ya
bahati” kilichopo Bwejuu.
Kutokana na umuhimu na faida ya kuweka akiba, baadhi ya vikundi
wamepandisha hisa zao kutoka shilingi 500 hadi shilingi 1000 na wengine kutoka
1000 hadi 2000 kwa hisa moja, hii ni kuonesha maendeleo na ukuwaji wa
wanavikundi hao ambapo mwanzoni kutokana na hali zao za kiuchumi
hawakutegemea kama wangeweza kumudu hata hiyo shingi 500 kwa hisa.
“Mwanzoni jamii na sisi wenyewe tulikua tuna mtazamo kwamba hatuwezi
kuweka akiba, na ilikua ni ngumu hata kuingia katika vikundi hivi kutokana na
kukosa hiyo shilingi 500 ya hisa, lakini baada ya kuingia na kumalizika mzunguko
wa mwanzo ile pesa tuloipata ilitusaidia sana, kwa hivyo tukakubaliana na
wenzangu kwamba madhali tushakua na biashara ndogo ndogo na ili faida iwe
kubwa mwisho wa mwaka, ni lazima tuongeze hisa kutoka shilingi 1000 hadi
shilingi 2000”, anasema Maryam Said ambae ni mshika fedha wa kikundi cha
“Tukiwezeshwa Tunaweza” kilichopo Mbuzini Pemba.
Vikundi hivi vimeanzishwa ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa iSAVE KIJALUBA
wenye lengo la kuwakomboa watu wenye ulemavu kiuchumi ambao unatekelezwa
na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA
ZNZ) na Shirikisho la Jumuiya za Watu wenye Ulemavu Zanzibar
(SHIJUWAZA), kwa ushirikiano mkubwa na Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu ya
Norway (NAD).
Dr. Mzuri Issa
Mkurugenzi
TAMWA ZNZ.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
PRESS RELEASE
42 Disability Groups Strengthen Economically Through iSAVE KIJALUBA
Members Benefit from Training and Loans
A total of TZS 143,077,862 has been collected in the first annual cycle from 42
iSAVE KIJALUBA savings and loan groups in the South District of Unguja and
Chakechake District of Pemba. These funds comprise shares deposited, community
fund money, and profits from loan management fees.
These groups have a total of 1,186 members, including 811 people with
disabilities, making up 68% of all members. Among these 811 members, 422 are
women and 389 are men.
Over the past year, these groups have received various types of training, including
business management training, savings and loan training, and training in the
production of various products such as soap, pickles, handicrafts, and vegetable
farming. These businesses have significantly helped them achieve economic
independence.
iSAVE KIJALUBA members are proud of these groups for promoting self-reliance
and supporting various activities, including their children’s education, business
development, household needs, and other expenses. Additionally, the community
fund has assisted them in times of disaster, bereavement, and other social issues.
“This group helps us a lot, and we are very proud of it. We do business, take loans,
and our lives have changed significantly. We are very grateful for the
establishment of these groups,” says Asha Amour, a member of the “Nyota ya
Bahati” group in Bwejuu.
Due to the importance and benefits of saving, some groups have increased their
share prices from TZS 500 to TZS 1,000, and others from TZS 1,000 to TZS 2,000
per share. This demonstrates the growth and progress of these group members,
who initially could not even afford the TZS 500 per share due to their economic
conditions.
“Initially, both the community and we had the perception that we could not save,
and it was even difficult to join these groups due to the lack of the TZS 500 for
shares. However, after joining and completing the first cycle, the money we
received helped us a lot. So, we agreed with my colleagues that since we already
have small businesses and to maximize our profits at the end of the year, we mustincrease the shares from TZS 1,000 to TZS 2,000,” says Maryam Said, the
treasurer of the “Tukiwezeshwa Tunaweza” group in Mbuzini, Pemba.
These groups were established as part of the iSAVE KIJALUBA project, aimed at
economically empowering people with disabilities. The project is implemented by
the Tanzania Media Women’s Association Zanzibar (TAMWA ZNZ) and the
Federation of Disabled People’s Organizations Zanzibar (SHIJUWAZA), in close
cooperation with the Norwegian Association of Disabled (NAD).
Dr. Mzuri Issa
Director
TAMWA ZNZ.