Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

ZAMECO KULAANI UTENGENEZWAJI NA USAMBAZWAJI WA MAUDHUI YASIOFAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

8/11/2024

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
ZAMECO KULAANI UTENGENEZWAJI NA USAMBAZWAJI WA MAUDHUI
YASIOFAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
Kamati ya wataalamu wa masuala ya Habari Zanzibar (ZAMECO) inayoundwa na Chama
cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA- Zanzibar), Baraza la Habari
Tanzania (MCT), Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA),
Jukwaa
la Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC Zanzibar) , Klabu ya
Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) pamoja na Klabu ya Waandishi wa Habari Pemba
(PPC) imelaani video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha wasichana
wawili wakirekodiwa na kuulizwa maswali yasio na maadili na yenye kuvunja heshima na
haki za binaadamu.
Tukio hili limeibua hisia kali kwa wadau wa habari, watetezi wa haki za binaadamu na
jamii kwa ujumla na kuibua maswali yasio na majibu miongoni mwa wanahabari kuhusu
maadili, haki za binadamu, na misingi ya uhuru wa vyombo vya habari.
Hivyo basi ZAMECO inasisitiza kuwa vitendo vya udhalilishaji kwa watoto wa kike na jamii
kwa ujumla ni ukiukwaji wa haki za binaadamu, maadili ya uandishi wa habari, na
kuvuruga mipaka ya uhuru wa kujieleza ambapo unalindwa na unahitajika kwa lengo la
kutoa habari sahihi na kuibua mijadala yenye tija na manufaa kwa jamii.
Kwa mujibu wa Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR 1996) Ibara
(19) “Kila mtu ana uhuru wa kutoa taarifa bila ya kuathiri haki ya mtu na amani ya nchi,”
hii ina maana kuwa uhuru wa vyombo vya habari unaendana na jukumu la kuheshimu
utu wa kila mtu, hasa wanawake na vijana, ambao ni waathirika wa moja kwa moja katika
hatari yoyote itakayotokea.ZAMECO inatoa msisitizo kwa mamlaka husika (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
pamoja na Tume ya Utangazaji Zanzibar kuhakikisha maudhui yanayorushwa na vyombo
vya habari na mitandao ya kijamii yanaendana na viwango vya maadili, uwajibikaji na
kuhakikisha kulinda jamii dhidi ya maudhui yenye madhara kwao, kama vile yaliyomo
yanayokiuka haki za binadamu, kudhalilisha, au kuchochea vurugu na chuki.
ZAMECO pia inaiomba Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Zanzibar
kuharakisha upatikanaji wa Sheria mpya ya Huduma za Habari nchini kwa lengo la
kupunguza changamoto kama hizo kwani ukizingatia katika mapendekezo ya sheria hiyo
(ambayo ni kilio cha muda mrefu kwa waandishi, wahariri na jamii kwa ujumla) imeelezea
kwa kina nani muandishi wa habari, sifa zake na kazi zake kwa ujumla.
Sambamba na hilo kamati ya wataalamu wa habari inatoa wito kwa mamlaka husika
kuchukuliwa hatua stahiki wale wote waliohusika kutengeza na kusambaza video hizo
zinazoharibu maadili haki za binadamu, na misingi ya uhuru wa vyombo vya habari katika
mitandao ya kijamii.
Aidha Kamati hiyo inasisitiza umuhimu wa wasichana kujitambua, kujithamini, na
kujiwekea malengo ambayo yatasaidia kuboresha maisha yao na jamii kwa ujumla kwani
wasichana wanapojitambua, wanakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi, kujiamini,
na kuepuka kutumiwa kwa maslahi ya wengine ambayo yanaweza kudhoofisha ndoto
zao.
ZAMECO pia inawaomba wazazi na walezi kuwa mstari wa mbele katika kuwaelimisha
watoto wao wa kike juu ya thamani yao, haki zao, na nafasi yao katika jamii
“ukimuelimisha mtoto wa kike ni sawa na kuielimisha jamii, sambamba na kuwaelimisha
vijana wa kiume kuwaheshimu watoto wa kike kwa kuwajengea mazingira yenye maadili
na heshima
Kamati ya wataalamu wa masuala ya Habari Zanzibar ZAMECO ipo tayari kushirikiana na
wadau wa sekta ya habari na Watetezi wa haki za binaadamu kuhakikisha kuwa matukio
kama haya hayajirudii tena, na kila mwandishi wa habari, mhariri, na mtangazajiwanaelewa na kutekeleza majukumu yao kwa njia inayolinda heshima, utu wa binadamu
na maadili ya uandishi wa habari.

Mwenyekiti ZPC Mkurugenzi TAMWA-ZNZ


Abdalla MfaumeDr. Mzuri Issa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00