04/11/ 2024.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
WAANDISHI WA HABARI WAJENGEWA UWEZO KUANDIKA HABARI ZA JINSIA NA MABADILIKO YA TABIANCHI
Jumla ya waandishi wa habari 30 kutoka vyombo vya habari mbalimbali ikiwemo magazeti, redio na mitandao ya kijamii watajengewa uwezo katika kuandika habari za Wanawake na uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Waandishi wahabari 20 kwa Unguja na 10 kwa Pemba watapatiwa mafuzo hayo ambayo yamelenga zaidi kuwapa waandishi ujuzi na maarifa ili kuandika habari sahihi na zenye kuleta uwajibikaji kwa makundi yote katika jamii, sambamba na kuangazia kwa undani jukumu muhimu la nafasi ya mwanamke na uongozi katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mafunzo haya yatafayika kwa siku mbili kuanzia tarehe 5 na 6 ya mwezi Novemba, ambayo yatakwenda sambamba kwa Unguja na Pemba. Waandishi watajengewa uwezo wa kuandika habari zenye kuzingatia sauti za wanawake kama viongozi katika suala zima la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, habari za uwajibikaji kwa makundi yote katika jamii, kufanya ufuatiliaji pamoja na habari zenye uchambuzi wa kina kuhusu sera, sheria na mikakati
mbalimbali ya kikanda na kimataifa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mafunzo hayo yamekuja kufuatia utekelezaji wa mradi wa ZanzAdapt, ambao ulianza na tathmini ya uchambuzi wa vyombo vya habari uliofanywa hivi karibuni na kugundua kuwa bado waandishi wa habari hawaandiki kwa kina habari za mabadiliko ya tabianchi, ambapo jumla ya habari 2,600 na vipindi 1,161 vya televisheni na redio vilivyochapishwa na kurushwa hewani kuanzia Jnauari hadi Mei, 2024 ni vipindi 11 (0.9%) pekee na habari 56 (2.1%) zilionyesha nafasi ya wanawake katika uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Aidha tathimni hiyo ilionyesha, jumla ya magazeti 608 yaliyoangaliwa kwa kipindi cha Jnauari hadi Mei, 2024 ambapo habari 34 (5.5%) tu zilionesha nafasi ya mwanamke na uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, zikizingatia masuala ya mabadiliko ya tabianchi ikiwemo mikoko na miti ya biashara na matunda.
Kufuatia tathimini hiyo ikaonekana kwamba kuna upungufu wa habari zenye kumuonyesha mwanamke katika nafasi uongozi na kazi anazofanya jamii hasa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Hivyo TAMWA-ZNZ, Community Forest Pemba (CFP) na Community Forest Intarnational (CFI) kwa kushirikiana na Serikali ya Canada, wanatekeleza mradi wa wanawake na uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Zanzibar (ZanzAdapt).
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
PRESS RELEASE:
JOURNALISTS EMPOWERED TO REPORT ON GENDER AND CLIMATE CHANGE ADAPTATION
A total of 30 journalists from various media outlets, including newspapers, radio stations, and social media platforms, will undergo capacity-building training to enhance their reporting on women leadership in addressing climate change adaptation.
The training will involve 20 journalists from Unguja and 10 from Pemba. It aims to equip them with skills and knowledge to produce accurate and impactful stories that promote accountability across all societal groups. Additionally, the training will emphasize the important role of women leadership in climate change mitigation efforts.
The two-day training will take place simultaneously in Unguja and Pemba on November 5th and 6th, 2024. Journalists will be trained to write stories that amplify women’s voices as leaders in combating climate change, focus on accountability across diverse groups, conduct effective follow-ups, and provide in-depth analyses of policies, laws, budget and strategies at regional and international levels in climate change adaptation.
This training initiative is part of the ZanzAdapt project, which began with a recent media gap analysis. The analysis revealed a lack of comprehensive reporting on climate change by journalists. Out of 2,600 news stories and 1,161 television and radio programs published or aired between January and May 2024, only 11 programs (0.9%) and 56 stories (2.1%) highlighted women’s leadership in climate change efforts.
Additionally, the analysis reviewed 608 newspapers during the same period, finding that only 34 stories (5.5%) featured women’s leadership in addressing climate change. These stories predominantly covered issues such as mangrove conservation and the cultivation of commercial and fruit trees.
The findings underscore a significant gap in reporting on women’s leadership and their contributions to societal efforts to climate change adaptation.
In response, TAMWA-ZNZ, Community Forest Pemba (CFP), and Community Forest International (CFI), in collaboration with Global Affairs Canada, are implementing the two years project namely “Zanzibar Women’s Leadership in Adaptation (ZanzAdapt) Project
Dkt. Mzuri Issa,
Mkurugenzi,
TAMWA ZNZ.