Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

NGUVU YA PAMOJA INAHITAJIKA KUFIKIA USAWA WA KIJINSIA KATIKA UONGOZI ZANZIBAR

NGUVU YA PAMOJA INAHITAJIKA KUFIKIA USAWA WA KIJINSIA KATIKA UONGOZI ZANZIBAR. mwenyekiti wa Bodi TAMWA ZNZ Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha waandishi wahabari Wanawake Tanzania, TAMWA ZNZ, Asha Abdi ameiomba jamii kuacha dhana potofu zinazorudisha nyuma juhudi za wanawake kogombea nafasi za Uongozi.
Akifungua maadhimisho ya siku ya wanawake yaliyofanyika katika Ofisi za TAMWA Tunguu , amesema nguvu ya jamii inahitajika kuwaunga mkono na kuwatetea wanawake wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi kwa lengo la kuleta usawa wa kijinsia katika ngazi za maamuzi.
“Tuwaunge mkono wanawake wanaowania nafasi za uongozi kwa kuwatia moyo, na kuwachagua ili kUfikia ili kufikia asilimia 50 si katika siasa tu bali katika michezo na nafasi nyengine’’ Bi Asha Abdi
Adha amesema historia inaonesha wanawake waliachwa nyuma katika harakati za kupigania uhuru kijamii, kisiasa na hata kichumi, jambo lilopelekea kudumaza maendeleo yao kwa muda mrefu.
Mapema Afisa Programu wa Michezo kwa maendeleo S4D kutoka TAMWA ZNZ, Khayrat Haji Ali amesema TAMWA ZNZ imeadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kuangalia changamoto zinazowakumba wanawake na wasichana katika sekta ya michezo, kushika nafasi za uongozi na kuzitafutia ufumbuzi.
Akiwasilisha Tathmini ndogo iliyofanywa na TAMWA ZNZ, Mtaalamu wa masuala ya Ufatiliaji na Tathmini kutoka TAMWA-ZNZ, Mohammed Khatib amesema Tathmini hiyo imegunduwa mapungufu kadhaa ikiwemo rasilimali fedha, ukosefu wa fursa na sera kutokuweka wazi na kufafanua mikakati maalum ya kumuwezesha mtoto wa kike kushiriki michezo na kushika nafasi za uongozi.
“Tuna sera nzuri ya michezo ina mikakakati mizuri lakini utekelezaji wake katika kuongeza nafasi za wanawake katika uongozi na fursa ndio tatizo” Mohammed Khatib, Mtaalamu wa Ufuatiliaji na tathmini TAMWA ZNZ.
Nae mshauri wa mambo ya Jinsia kutoka GIZ, Hijja Mohamed amesema kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wameandaa mikakati madhubuti ya kumuandaa mtoto wa kike kupata fursa na nafasi za uongozi kupitia michezo kwa kumuandalia mazingira salama na wezeshi.
Mwanamichezo Mkongwe kutoka Zanzibar Khatma Mwalim Khamis amesema, michezo sio uhuni bali ni kazi kama kazi nyengine ya kuingiza kipato, ila kupitia michezo wanakupambana na changamoto kadhaa ikiwemo masuala ya udhalilishaji jambo linalodumaza ndoto zao.
“Tunakwama kufikia hatua kubwa ya mafanikio na nafasi nzuri katika michezo kutokana na udhalilishaji na rushwa ya ngono kutokana na kujali utu wetu, hivyo ni muhimu tuwekewe mazingira rafiki ambayo yatachochea ufanisi katika michezo” Khatma Mwalim Mwanamichezo.
Aidha Katma Mwalim amewasihi wanawake kuingia katika michezo ili kujenga ukakamavu na afya bora.
Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 08 Machi, ambapo TAMWA ZNZ Imeadhimisha tarehe 21 Machi kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Marekani (GIZ).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00