Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

MAJAJI WAANZA KUCHAMBUA KAZI ZA WAANDISHI NA KUKAGUAVYOMBO VYA HABARI KWA AJILI YA TUZO ZA UWIANO WA KIJINSIA 2025

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAJAJI WAANZA KUCHAMBUA KAZI ZA WAANDISHI NA KUKAGUA
VYOMBO VYA HABARI KWA AJILI YA TUZO ZA UWIANO WA KIJINSIA
2025
Jopo la majaji waliobobea katika tasnia ya habari limeanza rasmi kuchambua kazi za
waandishi wa habari wanaowania Tuzo za Uwiano wa kijinsia kwa Vyombo vya
Habari kwa mwaka 2025.
Mbali ya kupitia kazi za waandishi, Majaji pia wameanza ukaguzi maalum wa
vyombo vya habari kuangalia namna vinavyopaza sauti za wanawake na kukuza
uandishi wa habari wenye kuzingatia uwiano wa kijinsia.
Tunatoa wito kwa vyombo vyote vya habari kujiandaa kuwapokea majaji, na kuwapa
mashirikiano katika kuhakikisha mchakato huu unaotekelezwa kwa ufanisi na uadilifu
mkubwa.
Kwa mwaka huu 2025 jumla ya kazi 120 za kihabari zimepokelewa kutoka vyombo
mbalimbali vya Habari ikiwemo magazeti, redio, televisheni na mitandao ya kijamii
Unguja na Pemba. Tofauti na miaka iliyopita, mwaka huu tunzo zimeshirikisha pia
vyombo vya Habari vyenyewe ili kuongeza ufanisi wa vyombo vya habari katika
masuala ya takwimu na wanawake na uongozi.
Mwelekeo huu mpya unalenga kutambua si tu ubora wa uandishi, bali pia juhudi za
ndani zinazofanywa na vyombo vya habari katika kuendeleza usawa wa kijinsia kupitia
sera zao, ratiba za vipindi, na mwelekeo wa kiuhariri.
Vigezo vinavyotumika katika tathmini kwa waandishi wa habari ni pamoja na:
•Ubunifu wa mada na upekee wa uwasilishaji
•Matumizi ya takwimu sahihi na vyanzo mbalimbali vya habari
•Mtazamo wa kijinsia na kuzingatia makundi ya pembezoni•Athari za kazi iliyochapishwa au kurushwa hewani katika jamii
•Maadili ya kitaaluma na ustadi wa lugha.
Vigezo vinavyotumika kwa vyombo vya Habari ni pamoja na:
•Uwepo na utekelezaji wa sera na madawati ya jinsia.
•Utekelezaji wa ufuatiliaji na tathmini wa masuala ya usawa wa kijinsia.
•Nafasi za wanawake katika ngazi za maamuzi ndani ya vyombo husika.
•Usalama na Ulinzi wa wanahabari.
Tunawahimiza waandishi na vyombo vya habari kuendelea kutumia kalamu zao kama
nyenzo ya kuleta mabadiliko. Ni kupitia habari zenye msingi wa takwimu, tafiti, na
ushahidi wa kijinsia ndipo tunaweza kuleta usawa wa kweli wa kijinsia katika uongozi.
Tuzo hizi ni sehemu ya utekelezaji wa program ya kuwawezesha wanawake katika
uongozi (SWIL), mradi unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya TAMWA ZNZ, ZAFELA,
PEGAO na JUWAUZA kwa mashirikiano na Ubalozi wa Norway nchini Tanzania.
Lengo ni kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi na kuimarisha
demokrasia jumuishi na shirikishi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari
TAMWA ZNZ, JUWAUZA, ZAFELA na PEGAO.
PRESS RELEASE
JUDGES BEGIN REVIEWING JOURNALISTS’ WORK AND ASSESSING MEDIA
OUTLETS FOR THE 2025 MEDIA FOR GENDER EQUITY AWARDS
A panel of seasoned judges in the media field has officially begun reviewing entries
submitted by journalists vying for the 2025 Media for Gender Equity Awards.
In addition to evaluating individual submissions, the judges have also commenced
special assessments of media outlets to examine how they amplify women’s voices
and promote gender-sensitive journalism.We call upon all media houses to prepare for and cooperate with the visiting panel,
ensuring the process is conducted with efficiency, professionalism, and integrity.
For the year 2025, a total of 120 journalistic entries have been received from various
media platforms, including newspapers, radio, television, and social media, from both
Unguja and Pemba. Unlike in previous years, this year’s awards have expanded to
include media institutions themselves, with the aim of enhancing the overall role of
media in promoting the use of data in stories related to women and leadership.
This new direction is intended to recognize not only the quality of journalism but also
the internal institutional efforts made by media houses to advance gender equity
through their policies, program schedules, and editorial strategies.
Evaluation criteria for journalists’ entries include:
•Creativity of the topic and uniqueness of presentation
•Use of accurate data and multiple sources
•Gender lens and inclusion of marginalized groups
•Social impact of the published or broadcasted work
•Professional ethics and language proficiency
Evaluation criteria for media outlets include:
•Existence and implementation of gender policies and gender desks
•Monitoring and evaluation of gender-related content and commitments
•Representation of women in decision-making roles within the institution
•Safety and protection of journalists
We encourage both journalists and media outlets to continue using their platforms as
tools for social transformation. It is through data-driven, research-based, and gender-
focused reporting that we can achieve true gender equality in leadership.
These awards are part of the Strengthen Women in Leadership (SWIL) program,
jointly implemented by TAMWA ZNZ, ZAFELA, PEGAO, and JUWAUZA in collaboration
with the Royal Norwegian Embassy in Tanzania. The goal is to increase women’s
participation in leadership positions and promote inclusive and participatory
democracy.Issued by:
TAMWA ZNZ, JUWAUZA, ZAFELA & PEGAO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00