Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI

MEI 14, 2025
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA ZAMECO
MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI
Zanzibar
Kamati ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar (ZAMECO) imesema Maadhimisho
ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani yanategemewa kufanyika Jumamosi tarehe 17 Mei,
2025 katika ukumbi wa RAHALEO STUDIO kuanzia saa 2:30 asubuhi ambapo
yatahudhuriwa na waandishi wa habari, wadau mbali mbali wa habari pamoja na
wawakilishi kutoka taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali.
Makamo mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. Mzuri Issa amesema kuwa maadhimisho ya
mwaka huu yana ujumbe muhimu na adhimu ambao ni “Sheria nzuri ya Habari ni
chachu ya uchaguzi ulio huru na wa haki”
Maadhimisho hayo ni muhimu katika kukuza na kuimarisha kada ya habari hapa nchini
pamoja na kutoa wito maalum kwa wadau wa habari kuhusu umuhimu wa kuwa na Sheria
mpya na rafiki yenye kusimamia mazingira salama kwa waandishi wa habari hasa
kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Aidha maadhimisho hayo yatatanguliwa na shughuli za kukuza na kuimarisha kada ya
habari ikiwemo kuandaa vipindi vya masuala ya uhuru wa habari pamoja na mikutano na
mafunzo kwa waandishi wa habari katika masuala ya sheria za habari. Pia kutakuwa na
mjadala kuhusu nafasi ya wanawake katika vyombo vya habari na umuhimu wa usawa
wa jinsia katika uongozi wa vyombo vya habari.
“Nia ya shughuli hizo ni kukuza weledi na umahiri wa waandishi wa habari katika masuala
ya sheria za habari ili watumie kalamu zao katika kufanya uchechemuzi wa sheria hizo,
na suala la kufuata weledi na umahiri katika kada ya habari litahimizwa”.
Kutakuwa na mijadala inayohusu umuhimu wa Sheria Mpya ya Huduma za Habari
Zanzibar, Ulinzi kwa Waandishi wa habari wakati wa uchaguzi na haki ya kuripoti bila
kubaguliwa katika uchaguzi. Lengo ni kuimarisha na kukuza kada ya habari nchini yenye
kuleta maendeleo na kuibua kero za wananchi.
“Mijadala pia italenga katika kuandika habari za makundi ya pembezoni pamoja na
kunyanyua sauti za wasio na sauti” Makamo Mwenyekiti alifafanua Zaidi.
Kamati ya maadhimisho ya kuandaa Siku ya Uhuru wa Habari hapa Zanzibar (ZAMECO),
inaundwa na taasisi na wadau wa habari ikiwemo Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya
Zanzibar (MCT ZNZ), Jukwaa la Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC-ZNZ),Chama cha Waandshi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ) , Jumuiya
ya Waandishi wa Habari za Maendeleo (WAHAMAZA) pamoja na Klabu ya Waandishi wa
Habari Zanzibar
MWISHO
Dkt. Mzuri Issa,
Mkurugenzi ,
TAMWA ZNZ
Abdallah Mfaume,
Mwenyekiti,
ZPC


May 14, 2025
PRESS RELEASE FROM ZAMECO
WORLD PRESS FREEDOM DAY COMMEMORATION
Zanzibar
The Zanzibar Media Committee (ZAMECO) has announced that this year’s World Press
Freedom Day celebrations will be held on Saturday, May 17, 2025, at RAHALEO
STUDIO, starting at 8:30 a.m. The event will bring together journalists, various media
stakeholders, as well as representatives from both government and non-governmental
institutions.
According the committee’s Vice Chairperson, Dr. Mzuri Issa, this years theme carries a
significant and noble message, “A good Media law is the catalyst for a free and fair
election”
These celebrations are crucial for promoting and strengthening the media sector in the
country. They also aim to deliver a special call to all media stakeholders on the importance
of enacting a new and friendly law that supports a safe working environment for
journalists especially as the country approaches the general elections scheduled for
October this year.
In the lead-up to the main event, there will be various activities aimed at enhancing and
developing the journalism profession. These include the production of special programs
on press freedom, as well as meetings and training sessions for journalists focusing onmedia law. There will also be a discussion on the role of women in the media and the
importance of gender equality in media leadership.
“The goal of these activities is to build the knowledge and professionalism of journalists
in media law so they can use their pens to advocate for these laws. Emphasis will be
placed on professionalism and integrity in the media industry,” said Dr. Mzuri.
Key discussions will revolve around:



The need for a New Media Services Law in Zanzibar,
Protection of journalists during elections.
The right to report impartially and without discrimination during the electoral
period.
The overall aim is to strengthen and grow a media sector that contributes to national
development and helps highlight citizens’ concerns.
“These discussions will also focus on reporting about marginalized groups and amplifying
the voices of the voiceless,” the Vice Chairperson elaborated.
The organizing committee for World Press Freedom Day in Zanzibar (ZAMECO) includes
institutions and stakeholders in the media sector, including Tanzania Media Women’s
Association, Zanzibar (TAMWA-ZNZ), Media Council of Tanzania, Zanzibar (MCT-ZNZ),
Tanzania Human Rights Defenders Coalition, Zanzibar (THRDC-ZNZ) Development
Journalists Association (WAHAMAZA) and Zanzibar Press Club (ZPC).
Dkt. Mzuri Issa,
Mkurugenzi ,
TAMWA ZNZ
Abdallah Mfaume,
Mwenyekiti,
ZPC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00