Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

Vyama vya siasa vyahimizwa kuzingatia ushirikishwaji wa watuwenye ulemavu kwenye mikutano ya kampeni.

05/10/2025
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Vyama vya siasa vyahimizwa kuzingatia ushirikishwaji wa watu
wenye ulemavu kwenye mikutano ya kampeni.
Taasisi zinazoshughulikia masuala ya uongozi wa wanawake vinaviomba vyama vya siasa
kuzingatia na kuhakikisha ushiriki wa watu wenye ulemavu katika mikutano ya kampeni
zinazoendelea ili kuweza kufuatilia sera zinazotolewa na wagombea wa vyama vya siasa
katika nafasi za Urais, Uwakilishi, Ubunge na Udiwani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba
2025.
Taasisi hizo ambazo ni pamoja na Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar
(JUWAUZA), Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO), Jumuiya ya
Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Chama cha Waandishi wa Habari
Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA-ZNZ) zimesema kuwa kuna baadhi ya vyama
havijazingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu katika mikutano yao jambo ambalo
linawanyima haki yao ya msingi ya kufuatilia sera za vyama na hivyo kufanya maamuzi
sahihi ya kura zao.
Katika taarifa ya pamoja taasisi hizo zimeeleza kuwa kuna baadhi ya vyama
vimeshuhudiwa vikiendesha mikutano ya kampeni bila ya kuandaa mazingira rafiki kwa
watu wenye ulemavu hali inayopelekea kushindwa kushiriki na kufuatilia kampeni
zinazoendelea kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
“Katika mikutano hiyo hukosekana kwa miundombinu wezeshi, ukosefu wa wakalimani
wa lugha ya alama, maandiko makubwa kwa wenye ulemavu wa macho, na vifaa vya
msaada wa kusikia ambapo huwanyima watu wenye ulemavu fursa ya kushiriki kikamilifu
katika mchakato wa kampeni muhimu katika mustakbali wa nchi”, imesema taarifa hiyo.Taarifa hiyo imesema kwa mfano ni chama kimoja tu ambacho kimeweka wakalimani
katika mikutano yake na ambao huonekana zaidi wakati wa mikutano inayofanywa na
mgombea wa Uraisi na hivyo katika nafasi nyengine mazingira hayo bado yanakosekana
isipokuwa kwa jimbo moja tu katika mkoa wa mjini magharibi ambapo kumeandaliwa
wakalimali maalum kwa ajili ya kundi hilo muhimu.
Taasisi hizi zinasisitiza vyama kuiga mfano huo wa wakalimani na kuhakikisha maeneo ya
mikutano yanafikika kwa urahisi, kuweka maandiko makubwa na vifaa vya msaada wa
kusikia katika maeneo yote katika mikutano yote ya wagombea wa Uraisi na nafasi
nyengine zikiwemo za Uwakilishi, Ubunge na Udiwani ili suala la ushiriki na ushirikishwaji
liwe na maana zaidi na kujenga demokrasia ya kweli.
Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) jumla ya watu wenye ulemavu
wapatao 8,021 wanatarajiwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 visiwani
Zanzibar.
Kwa mujibu wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (CRPD,
2006) Kifungu cha 9 kuwa nchi zihakikishe kuwa watu wenye ulemavu wanaishi kwa
kujitegemea na kuweka utaratibu wa kufikia huduma zote pamoja na mawasiliano na
teknolojia.
Sheria ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar Namba 8 ya mwaka 2022, kifungu cha 29
kinaeleza umuhimu wa watu wenye ulemavu kuweza kufikia miundo mbinu mbali mbali
pamoja, taarifa, mawasiliano na haki zote za kibinaadamu na za msingi.
Kutokana na haki walizopewa watu wenye ulemavu za kushiriki kikamilifu katika kampeni
za kisiasa, viongozi wa vyama vya siasa wanawajibika kuhakikisha ushiriki huo
unatekelezwa bila vikwazo kwa kuweka miundombinu rafiki katika viwanja vya kampeni,
kutoa taarifa zinazoweza kufikiwa kwa urahisi, na kuwezesha upatikanaji wa usafiri
pamoja na vifaa vya msaada.Aidha, Tume ya Uchaguzi na wadau wengine wanapaswa kutoa motisha kwa vyama na
wagombea wanaojumuisha watu wenye ulemavu, hatua ambayo itachochea usawa na
kudhihirisha mfano bora wa demokrasia jumuishi.
Imetolewa na
JUWAUZA, PEGAO, ZAFELA na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na Ubalozi wa
Norway nchini Tanzania ambao ni watekelezaji wa program ya kuhamasisha
wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi.

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00