



23/01/2026
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAMWA ZNZ, Community Forests Pemba na Community Forests International kuzindua Tuzo ya “Uandishi wa Habari za Tabianchi za ‘Community Forests”.
Kaulimbiu
“Kupaza Sauti za Wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi”.
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania – Zanzibar (TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na Community Forests Pemba (CFP) na Community Forests International (CFI) kupitia mradi wa Zanzibar Women’s Leadership in Adaptation(ZanzAdapt), tuna furaha kuwatangazia rasmi uzinduzi wa Tuzo “Uandishi wa Habari za Tabianchi za ‘Community Forests. Yenye kaulimbiu isemayo:“Kupaza Sauti za Wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi”.
Tuzo hizi zitatambua mchango wa waandishi wa habari na vyombo vya habari Zanzibar vinavyoandika, kurusha na kusambaza habari zinazooneshamchango wa wanawake na uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, hususan katika eneo la mikoko, kilimo mseto himilivu cha tabianchi (climate-smart agriculture) na kukuza usawa wa kijinsia kupitia kazi zao.
Malengo ya Tuzo
Kupitia tuzo hizi, TAMWA ZNZ, Community Forests Pemba na Community Forests international zinalenga:
- Kukuza uandishi wa habari unaoonyesha uongozi wa wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
- Kutambua mchango wa waandishi wa habari mahiri wanaoandika habari zinazohusu wanawake na uongozi kwenye masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
- Kuhamasisha uandishi wa habari unaozingatia usawa wa kijinsia, ushahidi wa kisayansi na hadithi za mabadiliko chanya kutoka ngazi ya jamii.
- Kuongeza uelewa wa jamii kuhusu mchango na uongozi wa wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Zanzibar.
- Kuweka mazingira ya ushindani kwa waandishi wa habari kuandika habari zenye ubora na athari chanya kuhusu wanawake na uongozi na mabadiliko ya tabianchi.
Kwa nini Tuzo hizi ni Muhimu:
Licha ya wanawake kuwa mstari wa mbele na kutoa mchango mkubwa katika shughuli za kilimo-misitu (agroforestry), uhifadhi wa mikoko, na mikakati mingine ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia mbinu za asili, lakini uongozi na mchango wao bado hauonekani vya kutosha katika vyombo vya habari na kwa jamii.
Uwakilishi mdogo wa wanawake katika simulizi za vyombo vya habari haupunguzi tu nafasi yao ya kushiriki na kuongoza, bali hupunguza mwonekano wa mikakati bora ya jamii katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Utafiti uliofanywa na mradi wa ZanAdapt Juni 2024 ulibaini kwamba, kati ya habari 4,548 kutoka vyombo vya habari mbalimbali ni asilimia 1.1 tu ya habari zilizojumuisha sauti za wanawake na wasichana, na asilimia 0.4 pekee zilizoonyesha wanawake kama viongozi katika muktadha wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mradi ZanzAdapt, unaotekelezwa na Community Forests International na Community Forests Pemba kwa ushirikiano na TAMWA Zanzibar, unalenga kuziba pengo hili kwa kuhamasisha uandishi wa habari unaozingatia usawa wa kijinsia na kutambua uongozi wa wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Ili kukabiliana na changamoto hii, Tuzo ya ““Uandishi wa Habari za Tabianchi za ‘Community Forests”.Yenye kaulimbiu isemayo “Kupaza Sauti za Wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi”. imeanzishwa kutambua mchango wa vyombo vya habari na kuhamasisha waandishi wa habari kuongeza juhudi katika kuandika habari za wanawake na uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Zanzibar.
Kupitia mradi wa ZanzAdapt, waandishi wa habari 30 (20 Unguja na 10 Pemba) pamoja na wahariri 20 wamejengewa uwezo kitaaluma ili waweze kuandika habari kwa ubora, ambapo wameweza kuandika habari zaidi 242 zinazozingatia uongozi wa wanawake katika kukabiliana na tabianchi. Tuzo hii inakuja kuthamini, kuendeleza na kuongeza juhudi hizo.
Tunzo hii itahusisha kazi zilizotolewa na waaandishi wa habari katika vyombo vya habari vya aina nne (4) kama ifuatavyo:).
- Uandishi wa makala katika magazeti (feature articles).
- Uandishi wa habari wa vipindi katika redio (radio program).
- Uandishi wa habari katika Televisheni (TV program).
- Uandishi wa makala katika mitandao ya kijamii (feature articles in social media)
Kazi zote lazima zionyeshe masuala ya mabadiliko ya tabianchi Zanzibar na ushiriki, sauti na uongozi wa wanawake Zanzibar.
Tuzo maalumu: Pia kutakuwa na tuzo maalum nne ambazo ni:
- Kutambua chombo cha habari kilichoonyesha uwajibikaji zaidi katika masuala ya wanawake na uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Hivyo vigezo vitakavyotumika ni kuangalia chombo cha habari kilichoongoza kuzalisha habari zenye ubora zilizorushwa au kuchapisha zinazohusu uongozi wa wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuonyesha jinsi kinavyolenga kuenzi na kuimarisha sauti za wanawake katika masuala ya tabianchi na uwiano wa kijinsia kati ya wafanyakazi.
- Tuzo ya mwandishi wa habari kijana wa habari za mabadiliko ya tabianchi (miaka 18-30). Vigezo kwamba mwandishi yoyote kijana, mwenye umri kuanzia miaka 18 hadi 30 anayefanya kazi katika chombo cha habari cha gazeti,television, redio na mitandao ya kijamii ambae ameandika habari inayohusu masuala ya wanawake na uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
- Tuzo ya uandishi wa habari wa mitandao ya kijamii. Vigezo ni kwamba kazi iwe imeangaliwa na watu wengi zaidi.
- Tuzo kwa habari iliyoangazia kwa ukubwa nafasi ya wanawake na uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Vigezo muhimu vya kuzingatia:
- Habari za Wanawake na uongozi katika mabadiliko ya tabianchi
- Umuhimu wa kuzingatia uwiano sawa wa jinsia
Usahihi wa taarifa na unaozingatia maadili ya uandishi wa habari - Ubora wa uandishi wa habari kwa picha (Visual Journalism Quality)
- Simulizi ya kipekee ya mada husika
- Ubunifu, uchunguzi bora wa mada
- Ufasaha na mtiririko wa lugha
- Ubora katika utayarishaji, sauti na uwasilishaji wa mada
- Ushawishi na ushirikishwaji wa hadhiara mitandaoni
- Vyanzo vingi vya habari.
Kipindi cha Redio na Television kisizidi dakika 30 na pia sauti na picha ziwe katika ubora unaostahiki.
Kwa Vyombo vya Habari Pekee:
- Dhamira ya chombo cha habari katika mabadiliko ya tabianchi
- Program zenye ubunifu na ushirikishwaji wa jamii
Vigezo kwa vyombo cha habari:
Chombo cha habari kinapaswa kuwasilisha andiko/maelezo ya kurasa mbili ikionyesha idadi na ubora wa habari au makala zilizochapishwa au kurushwa zinazohusu uongozi wa wanawake katika mabadiliko ya tabianchi, kuonyesha jinsi kinavyolenga kuenzi na kuimarisha sauti za wanawake katika masuala ya tabianchi, uwepo wa mwandishi wa habari maalum anayeshughulikia masuala ya mazingira na tabianchi miongoni mwa wafanyakazi wake, na uwiano wa kijinsia kati ya wafanyakazi. Vilevile, vyombo vya habari vinaweza kuweka taarifa nyingine yoyote wanayoiona inafaa ili kuimarisha maombi yao.
Mchakato wa Uwasilishaji na vigezo vya tahmini.
Dirisha la kupokea kazi liko wazi kwa waandishi wa habari wa Unguja na Pemba kutoka vyombo vya habari mbalimbali kutuma kazi zao, ikiwemo magazeti, televisheni, redio, na mitandao ya kijamii. Kazi zitakazopokelewa ni zile zilizochapishwa au kurushwa HEWANI kuanzia tarehe 01 Juni 2024 hadi tarehe 31 Disemba 2025, na lazima zihusishe:
- Masuala ya mabadiliko ya tabianchi Zanzibar;
- Wanawake na uongozi katika mabadiliko ya tabianchi Zanzibar
Maombi yamefunguliwa leo na kazi zitaanza kupokelewa kwa muda wa siku 21 kuanzia tarehe ya leo hadi tarehe 23 Januari hadi tarehe 14 Feburuari, 2026.
Waandishi wa habari mtatakiwa kuwasilisha kazi mbili (2) ambazo zimezalishwa, kuchapishwa na kurushwa HEWANI kwa kipindi kilichotajwa hapo juu kupitia kiungo/link itakayotumwa kwenye mitandao ya kijamii au kuleta moja kwa moja Ofisi za TAMWA ZNZ zilizopo Tunguu, Unguja na Mkanjuni Chakechake Pemba.
Jopo la majaji likiwa na wataalamu wa uandishi wa habari na jinsia,pamoja na wataalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi litapitia kazi zote zilizowasilishwa kwa umakini mkubwa mara tu baada ya kufungwa kwa zoezi la uwasilishaji na ukusanyaji kazi hizo.
Kazi zote zitakazowasilishwa zitapitia uhakiki wa awali wa jumla na majaji ili kuhakikisha zinakidhi vigezo vya msingi vifuatavyo:
- Lugha ya kazi iwe Kiswahili au Kiingereza.
- Mwandishi wa habari awe na umri wa miaka 18 au zaidi.
- Kazi iwe imechapishwa ndani ya kipindi kinachokubalika kwa mujibu wa kanuni za tuzo (kuanzia tarehe 1 Juni, 2024 hadi tarehe 31 Disemba, 2025).
- Kazi ijikite katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi Zanzibar.
- Kazi ionyeshe uongozi wa wanawake wa Kizanzibari.
- Kazi iwe katika moja ya makundi ya vyombo vya habari yaliyobainishwa.
- Mwandishi wa habari au chombo cha habari kiwe na makao yake Zanzibar.
- Kazi ikidhi vigezo vyote vya majaji.
Tarehe ya Tuzo:
Hafla ya utoaji wa tuzo inatarajiwa kufanyika tarehe 28 Machi 2026, kuanzia saa moja usiku katika hafla itakayowakutanisha waandishi wa habari, wahariri wa vyombo vya habari, wamiliki wa vyombo vya habari, taasisi za kiserikali, zisizo za kiserikali, za kimataifa na wanajamii.
Hitimisho:
TAMWA ZNZ, Community Forest Pemba na Community Forest International tunawakaribisha waandishi wa habari na vyombo vya habari vya Zanzibar kushiriki kikamilifu katika tuzo hizi, tuzo hizi ni jukwaa muhimu la kuonesha nguvu ya uandishi wa habari katika kuleta mabadiliko ya kijamii na kimazingira kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na sauti za wanawake na uongozi katika kukabiliana namabadiliko ya tabianchi ili kujenga uelewa kwa jamii na kuleta mabadiliko chanya.
Tuzo hizi ambazo ni mara ya kwanza kufanyika zimeandaliwa kupitia mradi wa Zanzibar Women’s Leadership in Adaptation (ZanzAdapt) kwa mashirikiano na Serikali ya Canada.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia: info@tamwaznz.or.tz & ngalapi@tamwaznz.or.tz.
Tuma maombi yako kupitia link hizi
- Mwandishi wa habari : https://docs.google.com/forms/d/e/1FAIpQLSe7bUAb8NuFngrwF8QMRvbI2WgViRX5k2_ziY5k7S5P3mI_ZA/viewform?usp=dialog
- Chombo cha habari : https://docs.google.com/forms/d/e/1FAIpQLSf1koBirzFta-uXp47ddGvVHKcdEO4sGjJZIPY9lPVwjo436Q/viewform?usp=dialog
PRESS STATEMENT
TAMWA Zanzibar, Community Forest Pemba, and Community International are launching the “Community Forests’ Climate Journalism Award.”
The theme is:
“Amplifying Women’s Voices in Climate Action.”
The Tanzania Media Women’s Association – Zanzibar (TAMWA ZNZ), in collaboration with Community Forests Pemba (CFP) and Community Forests International (CFI), through the Zanzibar Women’s Leadership in Adaptation (ZanzAdapt) project, is pleased to officially announce the launch of the Community Forests’ Climate Journalism Award under the theme “Amplifying Women’s Voices in Climate Action.”
This award will recognize the contributions of journalists and media outlets in Zanzibar who write, broadcast, and share stories highlighting the role of women and women’s leadership in responding to climate change. The focus areas include mangrove, climate-smart agriculture, and gender equality through their work.
The award objectives
- To promote the voice of women’s leadership in climate change adaptation journalism.
- To stimulate transformative journalism that informs empowers and drives gender responsive journalism across media platforms.
- To award journalists who have excelled in writing stories about women in leadership in climate change adaptation according to ZanzAdapt project.
- To increase awareness about women’s leadership in climate change adaptation in Zanzibar.
- To increase the visibility of women’s leadership voices and experiences in climate change adaptation discussions.
Why These Awards Are Important:
Despite women being at the forefront and making significant contributions to agroforestry, mangrove conservation, and other nature-based climate adaptation strategies, their leadership and contributions are still underrepresented in media and public discourse.
The limited representation of women in media narratives not only reduces their visibility and leadership opportunities but also diminishes awareness of effective community strategies for responding to climate change.
Research conducted by the ZanzAdapt project in June 2024 revealed that, out of 4,548 news stories from various media outlets, only 1.1% included women’s voices, and only 0.4% featured women as leaders in the context of climate change.
The ZanzAdapt project, implemented by Community Forests International and Community Forests Pemba in partnership with TAMWA Zanzibar, seeks to bridge this gap by promoting gender-sensitive journalism and recognizing women’s leadership in climate change response.
To address this challenge, the “Community Forests Climate Journalism Award,” under the theme “Amplifying Women’s Voices in Responding to Climate Change,” has been established to recognize media contributions and encourage journalists to increase their efforts in reporting on women and leadership in climate change in Zanzibar.
Through the ZanzAdapt project, 30 journalists (20 from Unguja and 10 from Pemba) and 20 editors have been professionally trained to produce high-quality stories, resulting in over 242 articles highlighting women’s leadership in climate action. This award seeks to honor, develop, and further motivate these efforts.
Award Categories:
The award will cover work submitted by journalists across four (4) types of media:
- Feature articles in newspapers
- Radio programs
- Television programs
- Feature articles on social media
All submissions must address climate change issues in Zanzibar and showcase women’s participation, voices, and leadership.
Special Awards: There will also be four special awards:
Outstanding Media House on Women and Climate Leadership
This award will recognize a media outlet that has demonstrated the highest level of accountability and commitment to reporting on women and leadership in climate change adaptation. The assessment criteria will include: the number and quality of stories produced and published or broadcast on women’s leadership in climate change adaptation, the outlet’s demonstrated commitment to amplifying women’s voices in climate-related issues, and gender balance among its staff.
Young Climate Change Journalist Award (Ages 18 – 30)
This award will recognize a young journalist aged between 18 and 30 years who work in print media, television, radio, or social media, and who has produced a story focusing on women and leadership in climate change adaptation.
Social Media Journalism Award
This award will be granted to a social media journalism piece that has reached and engaged the highest number of audiences.
Best Story on Women’s Leadership in Climate Change Adaptation
This award will recognize a story that has strongly and prominently highlighted the role and leadership of women in addressing climate change.
Key Evaluation Criteria:
- Quality work on women leadership and climate change.
- Importance of promoting gender balance and equality.
- Accuracy of information and adherence to ethical journalism standards.
- Quality of visual journalism (photography and video).
- A unique and compelling narrative on the selected theme.
- Creativity and strong investigative of the topic.
- Clarity and logical flow of language.
- Quality of production, sound, and overall presentation.
- Audience influence and engagement on digital platforms.
- Diversity of information sources.
Radio and television programs must not exceed 30 minutes, and both audio and visual quality must meet acceptable professional standards.
For Media Houses Only:
- Commitment to climate change reporting
- Innovative and community-engaging programs
Submission Guidelines and Evaluation:
The submission window is open to journalists from Unguja and Pemba across various media, including newspapers, television, radio, and social media. Eligible work must have been published or broadcast between 1 June 2024 and 31 December 2025, and must cover:
- Climate change issues in Zanzibar
- Women and leadership in climate change in Zanzibar
Applications open today, with submissions accepted for 21 days, from 23 January to 14 February 2026. Journalists are required to submit up to two (2) works produced, published, or broadcast during the stated period, either via a link shared on social media or delivered directly to TAMWA ZNZ offices in Tunguu, Unguja, and Mkanjuni Chakechake, Pemba.
A panel of judges, comprising journalism, gender, and climate change experts, will carefully review all submissions after the closing of the submission period. All submissions will undergo an initial general review by judges to ensure they meet the following minimum criteria:
- Language (Kiswahili or English)
- Age of journalists (over 18)
- Published within the award eligibility period (1st June 2024 – 31st December 2025)
- Focus on climate change issues in Zanzibar.
- Highlights Zanzibari women’s leadership.
- Categories of media.
- The journalist/media house must be based in Zanzibar.
- Must meet all judging criteria:
Award date:
The award ceremony is scheduled to take place on 28 March 2026, starting at 7:00 p.m., and will bring together journalists, media editors, media owners, government institutions, non-governmental and international organizations, as well as members of the community.
Conclusion:
TAMWA Zanzibar, Community Forests Pemba, and Community Forests International we welcome journalists and media houses in Zanzibar to participate in these significant awards. The awards provide an important platform to demonstrate the power of journalism in driving social and environmental change by promoting gender equality and amplifying women’s voices and leadership in climate change adaptation, thereby strengthening public awareness and fostering positive change.
These awards, which are being held for the first time, are organized under the Zanzibar Women’s Leadership in Adaptation (ZanzAdapt) project, in partnership with the Government of Canada.
For more information, please contact us at: info@tamwaznz.or.tz and ngalapi@tamwaznz.or.tz .
