CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE
T ANZANIA
P. O. Box 741 Tunguu Zanzibar,
Mobile No. 0772378378
Email: info@tamwaznz.or.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
13/03/2026.
JUWAUZA, PEGAO, ZAFELA, WEMA na TAMWA-ZNZ, wazindua Tuzo
ya uwiano wa kijinsia: “Kalamu Yangu, Mchango Wangu kwa
Wanawake.”
Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiya ya Wanasheria
Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba
(PEGAO), na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA
-ZNZ) kwa mashirikiano na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (WEMA
tuna furaha kutangaza rasmi uzinduzi wa Tuzo ya uwiano wa kijinsia kwa mwaka
2025/2026 yenye ujumbe unaosema “Kalamu Yangu, Mchango Wangu kwa
Wanawake.”
Tuzo hii itatambua waandishi wa habari na watengeneza maudhui (content creators)
wa Zanzibar wanaoandika na kuandaa maudhui ya kina yanayoangazia mafanikio,
changamoto na michango ya wanawake katika uongozi pamoja na kutatambua
wahamasishaji jamii waliofanya vizuri katika ngazi za wilaya kwa namna
wanavyoshiriki kikamilifu katika kukuza usawa wa kijinsia na kuhamasisha jamii kupitia
kazi zao.
Malengo ya Tuzo:
Kupitia tuzo hii, JUWAUZA, PEGAO, ZAFELA, WEMA na TAMWA ZNZ, wanalenga:
•
Kuhamasisha uandishi na utengenezaji wa maudhui unaokuza usawa wa
kijinsia.
•
Kukuza na kuimarisha uongozi wa wanawake katika sekta ya elimu.
•
Kukuza sauti za wanawake katika uongozi na maamuzi kwa ujumla
•
Kutambua mchango wa waandishi, wahamasishaji jamii na watengeneza
maudhui katika kuleta mabadiliko ya kijamii.
•
Kuimarisha uhamasishaji wa jamii kuhusu umuhimu wa wanawake kushiriki
katika uongozi na michakato ya kidemokrasia.
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tz
Utambuzi wa Waandishi, Wahamasishaji jamii na Watengenezaji wa
maudhui
Tuzo hii itahusisha kazi zilizotolewa katika makundi yafuatayo:
•
Uandishi wa habari za makala katika magazeti.
•
Vipindi vya redio.
•
Vipindi vya televisheni.
•
Makala au kampeni za mitandao ya kijamii.
Vigezo Muhimu vya Kuzingatia kwa waandishi wa Habari
•
Ubora wa kazi iliyowasilishwa.
•
Upekee wa mada.
•
Umuhimu wa kuzingatia uwiano sawa wa jinsia.
•
Vyanzo vingi vya habari vilivyojitawanya.
•
Ubunifu wa mada husika.
•
Matokeo baada ya kutoka kwa habari au kampeni hiyo (impact).
•
Uwasilishaji wa mada husika.
•
Mpangilio wa mada.
•
Ufasaha na mtiririko wa lugha.
•
Kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.
•
Uweledi na matumizi ya takwimu.
Kipindi cha Redio na Televisheni kisizidi dakika 30, na sauti pamoja na picha ziwe
katika ubora unaostahiki.
Kazi zinazowasilishwa lazima ziwe zimechapishwa au kurushwa hewani katika kipindi
cha kuanzia Januari 1 hadi Disemba 31, 2025.
Vigezo muhimu vya kuzingatia kwa watengenezaji wa maudhui (Content
Creators)
•
Ubunifu na uhalisia wa maudhui
•
Uelewa wa mada na kufikisha ujumbe kwa usahihi.
•
Ubora wa uwasilishaji maudhui kwa kutumia lugha, picha au video.
•
Uwezo wa maudhui kuhamasisha uelewa au mabadiliko chanya kwa jamii.
•
Kuhakikisha maudhui yanafuata maadili na yanatoa taarifa sahihi.
•
Maudhui yaliyosambaa na kuwafikia watu wengi.
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tz
Vigezo Muhimu vya Kuzingatia kwa wahamasishaji jamii (Citizen Brigades)
•
Kwa upande wa wahamasishaji wa
jamii tunaowatumia kuhamasisha jamii
kuhusu masuala ya wanawake na uongozi katika ngazi za chini, tuzo itatolewa
kwa wilaya mbili zitakazojitokeza kwa utendaji bora zaidi, wilaya moja kutoka
Unguja na wilaya moja kutoka Pemba.
•
Tathmini ya utendaji wao itazingatia kiwango cha juhudi za uhamasishaji
walizozifanya, kiwango cha ushiriki wa jamii,
•
Ubunifu wa mbinu walizotumia katika kufikisha ujumbe, pamoja na
•
Matokeo chanya yaliyojitokeza katika jamii kutokana na shughuli hizo.
•
Uwasilishaji wa ripoti za kazi zao kwa wakati.
•
Majaji wa kazi:
•
Katika kuhakikisha malengo ya tunzo hizi, kutakuwa na jopo la majaji ambalo
litakuwa na watu wenye sifa za ujuzi, uzoefu, usawa na uadilifu kutoka katika
maeneo yote yanayoangaliwa.
Washindi wote watatambuliwa na kupewa tuzo siku ya tarehe 02 Mwezi Mei 2026,
shughuli ambayo itawashirikisha pia wadau mbali mbali wa wanawake na uongozi.
Mchakato wa Uwasilishaji na Tathmini:
Maombi yamefunguliwa leo na kazi zitaendelea kupokelewa hadi tarehe 13 Aprili,
2026.
Kazi zinaweza kuwasilishwa moja kwa moja katika Ofisi za TAMWA ZNZ zilizopo
Tunguu – Unguja na Mkanjuni Chakechake – Pemba, au kupitia barua pepe ya
info@tamwaznz.or.tz pamoja na kiungo kitakachotumwa kwenye mitandao ya kijamii.
Hitimisho:
Huu ni msimu wa tano wa utoaji wa Tuzo hizi kupitia grogram ya kuwajengea
Wanawake uwezo katika Uongozi (SWIL) inayotekelezwa kwa mashirikiano na Ubalozi
wa Norway (RNE). Tuzo hizi ni mwendelezo wa jitihada za kuongeza ushiriki wa
wanawake katika uongozi na kuimarisha ushiriki wa kidemokrasia Zanzibar.
Mpaka sasa, jumla ya waandishi wa habari 53 pamoja na vyombo vya habari vitatu
vimetambuliwa kwa kuandika na kurusha maudhui yanayochangia kuongeza ushiriki
wa wanawake katika uongozi katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi 2024.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia info@tamwaznz.or.tz
au
ngalapi@tamwaznz.or.tz.
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tz
PRESS RELEASE
JUWAUZA, PEGAO, ZAFELA, WEMA and TAMWA-ZNZ Launch Media for
Gender Equity Awards: “My Pen, My Contribution to Women.”
Organization of Women with Disabilities in Zanzibar (JUWAUZA), Zanzibar Female
Lawyers Association (ZAFELA), Pemba Environment, Gender and Advocacy
Organization (PEGAO) and Tanzania Media Women Association, Zanzibar (TAMWA-
ZNZ), in collaboration with the Ministry of Education and Vocational Training (WEMA)
are pleased to officially announce the launch of the 2025/2026 Media for Gender
Equity Awards under the theme “My Pen, My Contribution to Women.”
These awards will recognize journalists and content creators from Zanzibar who
produce in-depth content highlighting the achievements, challenges, and contributions
of women in leadership. The awards will also recognize citizen brigades who have
performed well at the district level in promoting gender equality and mobilizing
communities through their work.
Objectives of the Awards
Through these awards, JUWAUZA, PEGAO, ZAFELA, WEMA and TAMWA ZNZ
aim to:
•
Encourage journalism and content creation that promotes gender equality.
•
Promote and strengthen women’s leadership in the education sector.
•
Amplify women’s voices in leadership and decision-making processes.
•
Recognize the contribution of journalists, citizen brigades, and content creators
in driving social change.
•
Strengthen community awareness on the importance of women’s participation
in leadership and democratic processes.
Recognition of Journalists, citizen brigades and Content Creators
The awards will consider work produced in the following categories:
•
Feature articles published in newspapers
•
Radio programs
•
Television programs
•
Social media articles or campaigns
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tz
Key Criteria for Journalists
Submissions will be evaluated based on:
•
Quality of the submitted work
•
Originality of the topic
•
Consideration of gender balance
•
Diversity of sources used
•
Creativity in presenting the topic
•
Impact of the story or campaign after publication/broadcast
•
Clarity of presentation
•
Organization and structure of the story
•
Fluency and coherence of language
•
Adherence to journalism ethics
•
Professionalism and use of data/statistics
Radio and television programs must not exceed 30 minutes, and the audio and visual
quality must meet acceptable standards.
Submitted work must have been published or broadcast between January 1 and
December 31, 2025.
Key Criteria for Content Creators
•
Creativity and authenticity of the content
•
Understanding of the topic and accuracy of message delivery
•
Quality of content presentation using language, images, or video
•
Ability of the content to inspire awareness or positive change in society
•
Adherence to ethical standards and provision of accurate information
•
Reach and engagement with a wide audience
Key Criteria for Citizen Brigades
Citizen Brigades who work at grassroots level to promote women’s leadership will also
be recognized.
•
Two districts will receive awards: one from Unguja and one from Pemba.
•
Their performance will be assessed based on:
Level of community mobilization efforts
Community participation
Creativity in communication approaches
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tz
Positive outcomes observed in the community
Timely submission of activity reports
Panel of Judges
To ensure the credibility of the awards, a panel of judges composed of individuals with
relevant expertise, experience, integrity, and balanced representation will evaluate the
submissions.
All winners will be recognized and awarded on May 2, 2026, during an event that will
also bring together various stakeholders working on women’s leadership.
Submission and Evaluation Process
Applications are open starting today, and submissions will be accepted until April 13,
2026.
Entries can be submitted:
•
Directly to TAMWA ZNZ offices in Tunguu – Unguja and Mkanjuni Chakechake
– Pemba, or
•
Via email at info@tamwaznz.or.tz, along with a link that will be shared on
social media platforms.
Conclusion
This is the fifth edition of these awards under the Strengthening Women in Leadership
(SWIL) program, implemented in collaboration with the Royal Norwegian Embassy
(RNE). The awards are part of ongoing efforts to increase women’s participation in
leadership and strengthen democratic participation in Zanzibar.
So far, 53 journalists and three media houses have been recognized for producing
content that contributes to increasing women’s participation in leadership between
2021 and 2024.
For more information, please contact us via:
info@tamwaznz.or.tz or ngalapi@tamwaznz.or.tz
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tz
