Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

Tuzo ya uandishi wa habari za Tabianchi za ‘Community Forestskufanyika kesho Jumamosi Machi 28,2026.

27/3/2026
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tuzo ya uandishi wa habari za Tabianchi za ‘Community Forests
kufanyika kesho Jumamosi Machi 28,2026.
 Ni Golden Tulip Hotel – Airport.
 Kuoneshwa mubashara ZBC TV
Community Forests Pemba (CFP), Community Forests International (CFI), na Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania – Zanzibar (TAMWA ZNZ) wanayo furaha
kuwajuilisha umma kwamba hafla ya kutoa Tuzo za Uandishi wa Habari za Tabianchi za
“Community Forests” itafanyika kesho, Jumamosi, tarehe 28 Machi 2026 kuanzia saa
12:00 jioni, katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport, Unguja.
Tuzo hizo zenye kauli mbiu “Kupaza Sauti za Wanawake katika kukabiliana na
mabadiliko ya tabianchi” zina lengo la kutambua mchango wa waandishi na vyombo
vya habari Zanzibar vinavyoandika, kurusha na kusambaza habari zinazoonesha mchango
wa wanawake na uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, hususan katika
eneo la mikoko, kilimo mseto himilivu cha tabianchi (climate-smart agriculture) na kukuza
usawa wa kijinsia kupitia kazi zao.
Hafla hiyo itawaleta pamoja washiriki 140 kutoka sekta ya habari, taasisi za kiserikali na
jumuiya zisizokuwa za kiraia kutoka Unguja na Pemba, wakiwemo waandishi wa habari
kutoka vyombo mbalimbali vya habari ambao ndio walengwa wa tuzo hizo watashiriki.
Aidha, hafla hiyo ya tuzo itaoneshwa moja kwa moja kupitia Televisheni ya ZBC pamoja
na televisheni za mtandaoni (online TV), lengo ni kutoa fursa kwa jamii kuweza kufuatilia
utoaji wa tuzo kwa waandishi na vyombo vya habari vya Zanzibar kwa kazi zao bora
zinazohusiana na uongozi wa wanawake katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.
Tuzo za Community Forests ni mara ya kwanza kufanyika, ambapo jumla ya kazi 73 za
waandishi na vyombo vya habari Zanzibar ziliwasilishwa kwa ajili ya kuwania tuzo hizo.
Miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na vipindi vya radio, televisheni, makala za magazeti
na zile kutoka katika mitandao ya kijamii zilizoandikwa na kurushwa katika vyombo
mbalimbali vya habari kuanzia mwezi Juni 2024 hadi Disemba 31, 2025.
Tuzo hizi ni jukwaa muhimu la kuonesha nguvu ya uandishi wa habari katika kuleta
mabadiliko ya kijamii na kimazingira kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na sauti za
wanawake na uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kujenga uelewa
kwa jamii na kuleta mabadiliko chanya.
Tuzo ya uandishi wa habari za Tabianchi za Community Forests zimeandaliwa kwa pamoja
na Community Forests Pemba (CFP), Community Forests International (CFI) na Chama
cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), kwa kushirikiana
na Serikali ya Canada.
Imetolewa na
Kitengo cha habari
TAMWA –Zanzibar.

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00