Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

BONANZA LA MICHEZO NA MAZOEZI KUFANYIKA PEMBA

BONANZA LA MICHEZO NA MAZOEZI KUFANYIKA PEMBA

BONANZA LA MICHEZO NA MAZOEZI KUFANYIKA PEMBA: JULAI20 – 28, 2024
Katika kuadhimisha miaka 10 ya klabu ya mazoezi ya Gombani
(Gombani Fitness club), klabu hiyo kwa kushirikiana naChamaChaWaandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA-ZNZ)na Shirika ka Bima la Zanzibar wameandaa bonanza lamchezowamazoezi lenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa wanawakenawasichana katika mazoezi na michezo. Bonanza hilo litakaloshirikisha michezo ya aina mbali mbali
litafanyika kisiwani Pemba kuanzia tarehe 20 hadi 28, Julai mwakahuu. Viongozi mbali mbali wa serikali na taasisi binafsi
wanatarajiwa kushiriki siku ya Jumapili ya tarehe 28 ambayondioitakua kilele cha maadhimisho hayo kwa kuanza namatembezi
kutoka Madungu na kumalizikia katika Uwanja waMpirawaGombani, kuanzia saa 12:00 asubuhi. Jumla ya michezo mitatu itachezwa siku hiyo ikiwemomazoezi yaviungo, mchezo wa magunia na mchezo wa kuvuta kambaambayojinsia zote zitashiriki kwa kuonesha vipaji na uwezo wao. Katika shamrashamra za kuelekea kilele cha maadhimishohayowaandaaji wa bonanza hilo watapita skuli na shehia mbali mbali
kuhamasisha kuhusu usawa wa kijinsia katika mazoezi namichezo,pamoja na kuwafundisha wanafunzi jinsi ya kujikinga naukatili wa
kijinsia (GBV) kupitia michezo maalum inayojulikana kama(S4Dacitivities). Aidha jumla ya washiriki 500 kutoka maeneo mbali mbali yaUnguja, Pemba na Tanga wanatarajiwa kushiriki katikamaadhimisho hayo ambapo kauli mbiu ni “Wekezakatikamazoezi na michezo kwa jinsia zote”. Kauli mbiuhii inabebalengo la bonanza hili kwa kuhakikisha watu wote wanahamasikakushiriki katika michezo bila kujali jinsia zao. Kwa kushirikiana na Shirika la Bima la Zanzibar tunahamasishaWanamichezo kujikatia bima ya ‘Group Personal Accident’ (Bimaya ajali kwa Wanakikundi) ambayo itakuwa inawakingadhidi yamaumivu ya mwili na/au vifo vitakavyosababishwa naajali wakati
wakiwa katika mazoezi na harakati zao za michezo za kilasiku. Wakati Gombani Fitness Club inatimiza miaka 10 tokeakuanzishwakwake, mafanikio kadhaa yamepatikana ikiwemo kuimarikakwaafya za wana klabu, bado kuna changamoto mbali mbali ikiwemokutokuwepo kwa miundombinu rafiki ya kufanyia mazoezi kisiwani
Pemba hususani kwa wanawake, dhana potofu dhidi yamazoezi yaviungo, na kukosekana kwa taarifa sahihi juu ya umuhimuwamazoezi na michezo katika vyombo vya habari. Kwa sasa TAMWA ZNZ inatekeleza programu ya michezokwamaendeleo yenye lengo la kukuza usawa wa kijinsia katikamichezoambayo inatekelezwa kwa pamoja na Jumuiya ya WanasheriaWanawake Zanzibar (ZAFELA), Kituo cha Mijadala kwaVijana(CYD) kwa ushirikiano mkubwa na Taasisi ya Maendeleoyakimataifa ya Ujerumani (GIZ). Imetolewa na;
Kamati ya maandalizi,
Bonanza la Michezo na Mazoezi Pemba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00