Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

Vikundi 16 Vyajengewa Uwezo wa Kuchagua Biashara zenye Tija

11/09/2025

Jumla ya wanachama 25 kutoka vikundi 16 vya kuweka na kukopa katika Wilaya ya Kusini Unguja wamepatiwa mafunzo ya siku mbili ya kuchagua, kupanga na kusimamia biashara, chini ya Programu ya Mashirikiano ya Pamoja kwa ajili ya Haki za Watu wenye Ulemavu (CADiR) inayotekelezwa na Chama cha waandishi wa Habari wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), Shirikisho la Jumuiya za Watu wenye Ulemavu Zanzibar (SHIJUWAZA) na Jumuiya ya wasioona Zanzibar (ZANAB) kwa ushirikiano mkubwa na Shirika la Watu Wenye Ulemavu la Norway (NAD).

Washiriki hao ambao 16 ni watu wenye ulemavu na 9 ni walezi na wasimamizi wa Watoto wenye ulemavu wamehudhuria mafunzo kama wawakilishi wa vikundi vyao, na wanatarajiwa kuyafikisha maarifa haya kwa wanachama wenzao, ili kila kikundi kinufaike kwa pamoja na kuimarisha biashara zake.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Aziza Ismail ambae ni Mratibu wa program ya CADiR kutoka NAD, amesema taasisi zinazoshirikiana katika programu hii zina matumaini makubwa kuwa mafunzo haya yatawawezesha wawakilishi wa vikundi kupeleka elimu waliyoipata kwa wenzao, hatimaye kusaidia wanachama wote kuchagua biashara bora na zenye tija.

“Kwa vile miongoni mwa malengo makuu ya program hii ni kuwawezesha watu wenye ulemavu kuinuka kiuchumi na kupata kipato rasmi, tunaamini mafunzo haya yatasaidia kikamilifu kulifikia lengo hili”, alisisitiza Mratibu huyo.

Mkufunzi wa mafunzo hayo, Muhidini Ramadhan kutoka TAMWA ZNZ amesema kuwa hali ya umasikini inaweza kupungua kwa watu wenye ulemavu iwapo wataelimishwa juu ya ujuzi na miradi ya kiuchumi yenye tija.

Nae Meneja wa Programu kutoka TAMWA ZNZ Nairat Ali, amesema mafunzo haya ni muhimu kwa ajili ya kuwasaidia wanachama kupanga na kuchagua biashara zenye tija ili vikundi viwe endelevu na viweze kujitegemea kiuchumi.

Kwa upande wake ndugu Khamis Ali, Afisa Program kutoka ZANAB, amewataka washiriki wa mafunzo hayo kujifunza kwa umakini mafunzo hayo ili waweze kuchagua biashara sahihi zitakazowawezesha kupata mikopo na kuweza kurudisha kwa wakati.

Washiriki walijadili na kuandika mipango ya biashara, baadhi wakieleza ndoto zao za kukuza biashara ndogondogo walizonazo, ikiwemo kilimo, ufugaji, kufungua maduka na ushonaji.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake, Yusra Ali Hassan ambaye ni Msaidizi Katibu wa kikundi cha Mtu ni Utu cha Kajengwa, ameshukuru waandaaji wa mafunzo hayo na kusema yamewapa muongozo mzuri wa namna ya kupanga biashara na kutumia vizuri fedha katika kukuza biashara zao.

Kupitia mafunzo haya tumejifunza kupanga matumizi kwa uangalifu na kuweka mipango thabiti ya biashara, binafsi nimeona namna biashara ya ushonaji inavyoweza kukua zaidi nikiwa na maarifa haya mapya,” amesema Yusra.

Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika katika ukumbi wa walimu Kitogani ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa program ya CADiR katika eneo la uwezeshaji kiuchumi ambalo linalenga kuanzisha na kuimarisha vikundi vya watu wenye ulemavu vya kuweka na kukopa katika wilaya 11 za Unguja na Pemba.

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00