Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UDHALILISHAJI WA KIJINSIAZANZIBAR

05/12/2025
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA
ZANZIBAR
“Tathmini ya ushiriki wa wanawake, watu wenye ulemavu na vijana katika
Uchaguzi Mkuu wa 2025”
Taasisi zinazotetea haki za wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na watoto Zanzibar
kesho Jumamosi tarehe 06 Disemba 2025 zitaungana kwa pamoja kuadhimisha Siku 16
za Kupinga Udhalilishaji wa Kijinsia katika hafla maalum itakayofanyika katika Ofisi za
TAMWA Zanzibar, Tunguu.
Katika hafla hiyo itawasilishwa ripoti ya maoni ya wadau juu ya kuangalia nafasi ya
mwanamke katika uchaguzi mkuu uliopita kwa mtazamo wa usawa wa kijinsia ikiwemo
ushiriki jumuishi na wenye usawa kwa makundi yote katika mfumo wa kisiasa ambapo
itaangalia mafanikio, changamoto na mwenendo wa haki za wanawake, vijana na watu
wenye ulemavu katika mazingira ya kisiasa na ya kidijitali.
Hafla hii inatarajiwa kuwakutanisha wadau 80 kutoka taasisi za kiserikali, zisizo za
kiserikali, pamoja na waandishi wa habari kwa lengo la kuongeza uelewa na kuimarisha
mbinu za pamoja za kukabiliana na udhalilishaji wa kijinsia katika zama za mabadiliko
ya teknolojia na taarifa.Taasisi zinazoanda maadhimisho haya ni Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu
Zanzibar (JUWAUZA), Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), Pamoja Youth
Initiative (PYI), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Jumuiya ya
Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO), Jumuiya ya Kupambana na Changamoto
za Vijana Zanzibar (ZAFAYCO), Jukwaa la Vijana Zanzibar (ZYF), Mtandao wa watetezi
wa haki za binaadam Tanzania (THRDC) pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari
Wanawake Tanzania,Zanzibar (TAMWA ZNZ).
Mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania ikiwemo Zanzibar imeridhia
inasisitiza kulinda na kuendeleza haki za wanawake na watoto, mikataba hiyo ni pamoja
na Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Uonevu Dhidi ya Wanawake (CEDAW), Itifaki
ya Maputo inayotetea haki za wanawake barani Afrika; Azimio la Beijing (1995)
linalosisitiza ushiriki wa wanawake katika uongozi, pamoja na Malengo ya Maendeleo
Endelevu (SDGs), hususan Lengo namba tano linalolenga usawa wa kijinsia na
kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.
Ujumbe wa Kimataifa kwa mwaka 2025 ni “TUUNGANE Kukomesha Ukatili wa Kidijitali
Dhidi ya Wanawake na Wasichana”, huku ujumbe wa kitaifa ukiwa “Mitandao Salama ni
Haki: Maliza Ukatili wa Kimtandao kwa Wanawake na Watoto.” Ujumbe huu unasisitiza
umuhimu wa kuhakikisha matumizi salama ya teknolojia, kuimarisha mifumo ya
kudhibiti na kuripoti ukatili wa mtandaoni, na kulinda haki za wanawake na wasichana
kwenye majukwaa ya kidijitali.
Kampeni ya Siku 16 ni harakati ya kimataifa iliyoanzishwa mwaka 1991 inayolenga
kuhamasisha hatua za kukomesha ubaguzi na ukatili wa kijinsia. Maadhimisho huanza
tarehe 25 Novemba, Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake, na
kuhitimishwa tarehe 10 Disemba siku ya Haki za Binadamu Duniani huku ikisisitiza
kwamba udhalilishaji wa kijinsia ni ukiukwaji wa haki za Binadamu.Kampeni hii huhamasisha mabadiliko ya sera, elimu kwa umma, utafiti na hatua za
pamoja za kukomesha ukatili wa kimwili, kijinsia, kisaikolojia, kiuchumi na sasa ukatili
wa kidijitali ambao unaongezeka duniani kote.
Imetolewa na:
Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA)
Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC)
Pamoja Youth Initiatives (PYI)
Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA)
Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO)
Jumuiya ya Kupambana na Changamoto za Vijana Zanzibar (ZAFAYCO)
Jukwaa la Vijana Zanzibar (ZYF)
Mtandao wa watetezi wa haki za binaadam Tanzania (THRDC)
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA
ZNZ).

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00