Edit Content

About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

TAMWA ZNZ Kuadhimisha Siku ya Redio Duniani.

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE
TANZANIA
P. O. Box 741 Tunguu Zanzibar, TEL: 0242232263
Mobile No. 0772378378

Email: info@tamwaznz.or.tz

10/02/2025.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAMWA ZNZ Kuadhimisha Siku ya Redio Duniani.
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania – Zanzibar (TAMWA ZNZ)
kitaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Redio kwa kukutana na wadau mbalimbali wa habari ili
kutathmini mchango wa redio na mchango wa TAMWA katika kuhabarisha, kuhamasisha
maendeleo na kuchochea mijadala yenye tija kwa jamii.
Hafla hii itafanyika tarehe 12 Februari katika ofisi za TAMWA ZNZ Tunguu, na
itawakutanisha wadau kutoka sekta ya habari kwa Unguja na Pemba, wakiwemo viongozi wa
vyombo vya habari, wahariri, wakuu wa vipindi, pamoja na waandishi wa habari. Kauli mbiu
ya mwaka huu ni “Redio na Mabadiliko ya Tabianchi”, ikilenga kuangazia namna redio
inavyoweza kusaidia katika kuelimisha jamii kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi na njia
za kukabiliana nazo.
Katika muktadha wa mabadiliko ya tabianchi, redio inachukua jukumu muhimu katika kutoa
elimu kwa jamii kuhusu athari za tabianchi, mbinu za kukabiliana nazo, na umuhimu wa
uhifadhi wa mazingira. Kupitia vipindi vya redio, jamii inapata taarifa kuhusu mabadiliko ya
hali ya hewa, mbinu za kilimo kinachohimili ukame, na njia za kupunguza uchafuzi wa
mazingira.
Aidha kupitia Kaulimbiu hii TAMWA ZNZ inaviomba vyombo vya habari kuandika habari
za wanawake na uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kwani tafiti za hapa
Zanzibar zinaonyesha kwamba sauti za wanawake hazipewi nafasi ipasavyo katika vyombo
vya habari.
Utafiti uliofanywa na TAMWA ZNZ mwaka 2024 ulionyesha kwamba jumla ya vipindi 2600
viliandaliwa na kurushwa hewani na ZBC na Assalam Radio ambapo kati ya hivyo 11 pekee
ndivyo vilivyohusu mabadiliko ya tabianchi ambayo ni sawa na asilimia (0.9%).
TAMWA ZNZ inatambua mchango mkubwa wa wanahabari kupitia redio katika kuhakikisha
jamii inapata taarifa sahihi kwa wakati. Redio imeendelea kuwa chombo madhubuti cha
kuelimisha jamii kuhusu haki za wanawake na watoto, usawa wa kijinsia, ushiriki wa
wanawake katika uongozi, na kujenga uelewa katika katika kukabiliana na vitendo vya
udhalilishaji wa kijinsia.
Kwa ushirikiano wa karibu na vyombo vya habari, TAMWA ZNZ imefanikiwa kutoa jumla
ya habari 778 kwa mwaka 2024 kupitia programu mbalimbali na vyombo tofauti vya habari.
Kati ya hizo, habari 502, zilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii, 120 kwenye magazeti,
101 kwenye redio, na 55 kwenye televisheni.
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tzMiongoni mwa hizo, habari 325 zilihusiana na program za Udhalilishaji, Afya ya Uzazi na
Michezo kwa Maendeleo, 204 zilihusu Uhuru wa Habari na Kujieleza, 225 zilihusu
Wanawake na Uongozi, na 24 zilihusu Kuwainua Wanawake Kiuchumi. Ushirikiano huu
umewezesha uhamasishaji mkubwa wa jamii na kuleta mijadala muhimu katika kupinga
ukatili na kuhimiza usawa wa kijinsia, na kusaidia wanawake kushiriki kikamilifu katika
maendeleo ya taifa.
Kwa mnasaba huu, TAMWA ZNZ inatoa shukrani kwa vyombo vyote vya habari pamoja na
wanahabari kwa mchango wao wa dhati katika kuhakikisha vyombo vya habari ikiwemo
redio vinaendelea kuwa vyombo vyenye nguvu na kuchangia kuleta mabadiliko chanya
katika jamii.
Redio inaendelea kuwa chombo muhimu cha mawasiliano kinachofikia watu wengi kwa
urahisi, hata wale walioko katika maeneo ya pembezoni ambako vyombo vingine vya habari
haviwezi kufika kwa urahisi.
TAMWA,ZNZ inazipongeza redio zote kwa mchango mkubwa katika kutoa taarifa kwa
wananchi na inaungana nazo katika kuadhimisha siku hiyo adhimu na kuvitakia kila la kheri
katika mipango yake ya baadae.
Siku ya Kimataifa ya Redio huadhimishwa kila mwaka Februari 13 kwa lengo la kutambua
mchango wa redio katika kufikisha taarifa kwa jamii. Mwaka 2011, Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lilitangaza rasmi siku hii, na mwaka
2013, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa likaipitisha kama tukio la kimataifa.
Dkt. Mzuri Issa,
Mkurugenzi,
TAMWA ZNZ.
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tz

PRESS RELEASE
TAMWA ZNZ to Commemorate World Radio Day.
Tanzania Media Women’s Association,Zanzibar (TAMWA ZNZ) will commemorate World
Radio Day by bringing together various media stakeholders to assess the role of radio and
TAMWA’s contribution in informing the public, promoting development, and fostering
meaningful discussions in society.
This event will take place on 12th February at TAMWA ZNZ offices – Tunguu and will bring
together including Media Executives, Editors, Heads of Programs, and Journalists. This
year’s theme, “Radio and Climate Change,” aims to highlight how radio can play a vital
role in educating communities about the effects of climate change and ways to mitigate them.
In the context of climate change, radio plays a crucial role in educating communities about its
impacts, adaptation strategies, and the importance of environmental conservation. Through
radio programs, communities receive information about weather changes, climate-resilient
farming techniques, and ways to reduce environmental pollution.
Additionally, under this theme, TAMWA ZNZ urges media outlets to cover stories about
women and leadership in tackling climate change, as research in Zanzibar shows that
women’s voices are not sufficiently represented in the media.
A 2024 study conducted by TAMWA ZNZ revealed that out of 2,600 programs broadcasted
by ZBC and Assalam Radio, only 11 focused on climate change, representing just 0.9% of
the total content.
TAMWA ZNZ recognizes the significant contribution of journalists and radio in ensuring
communities receive accurate and timely information. Radio continues to be a powerful tool
in educating the public about women’s and children’s rights, gender equality, women’s
participation in leadership, and raising awareness on Gender Based Violence (GBV).
Through close collaboration with media outlets, TAMWA ZNZ successfully published a total
of 778 news stories in 2024 through various programs and media platforms. Of these, 502
were published on social media, 120 in newspapers, 101 on radio, and 55 on television.

Among these stories:
325 covered programs on GBV, reproductive health, and sports for development.
204 focused on freedom of expression and press freedom.
225 addressed women’s leadership.
24 highlighted women’s economic empowerment.
This collaboration has facilitated widespread public awareness, fostered essential discussions
on combating violence, and promoted gender equality, encouraging women’s full
participation in national development.
On this occasion, TAMWA ZNZ extends its gratitude to all media houses, as well as
journalists, for their dedication in ensuring that the media, including radio, remains a
powerful platform for positive social change.
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tzRadio remains a crucial communication tool, reaching a broad audience, including those in
remote areas where other forms of media may not easily access.
TAMWA ZNZ commends all radio stations for their significant role in providing information
to the public and joins them in celebrating this important day, wishing them success in their
future endeavors.
World Radio Day is observed annually on 13th February to recognize radio’s role in
disseminating information to communities. In 2011, the United Nations Educational,
Scientific and Cultural Organization (UNESCO) officially declared this day, and in 2013, the
United Nations General Assembly adopted it as an international event.

Dr. Mzuri Issa,
Director,
TAMWA ZNZ
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00