
CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE
TANZANIA
P. O. Box 741 Tunguu Zanzibar, TEL: 0242232263
Mobile No. 0777479858
Email: info@tamwaznz.or.tz
18/02/2025.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
TAMWA ZNZ yataka waliohusika na tukio la ukatili kwa
mwanamke waadhibiwe
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA
ZNZ) inasikitishwa na tukio la hivi karibuni lililotokea Unguja, ambapo
imedaiwa kuwa Bi. Khadija Shaaban Ali (34) alimshambulia na kumjeruhi mke
mwenzake kwa kumpiga visu, Bi Maimuna Said Suleiman (38), tukio
lililomsababishia maumivu na majaraha makubwa.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka vyombo mbalimbali vya habari, ikiwemo ZBC
Radio kupitia kipindi cha Habari za Mawio kilichorushwa hewani tarehe 11
Februari 2025 ni kuwa wanawake hao walikuwa wamepakiwa katika gari moja
na mume wao hadi nyumbani kwa mke mdogo huko Chukwani, mkoa wa mjini
magharibi.
Kwa mujibu wa mawio mume aliingia ndani na kuwaacha wake zake hao
wawili peke yao na ndipo mkasa huo ukaanza kutokea, ambapo taarifa zinadai
kuwa Bi Maimuna alianza kupigwa kwa visu na kupiga makelele ya kuomba
msaada lakini hata mumewe hakuweza kutoka kwa wakati.
TAMWA, ZNZ inasikitishwa na tukio hilo la Bi Khadija kumshambulia mke
mwenziwe vibaya na kumsababishia madhara makubwa ya kimwili.
TAMWA ZNZ inasikitika zaidi na kitendo hicho cha mume wa wake hao
kuondoka na kuwaacha peke yao bila ya hadhari zozote wakati yeye anawajua
tabia zao vya kutosha.
Aidha inasisitiza kuwa hatua kali za kisheria zinahitaji kuchukuliwa dhidi ya
wote waliohusika na kadhia hiyo ili iwe funzo kwa watu kujichukulia sheria
mikononi mwao.
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tzTAMWA ZNZ inatoa ushauri kwa Serikali kuangalia uwezo wa wanaume
wanaooa wake zaidi ya mmoja kama wana uwezo wa kutosha wa kuwahudumia
na kuwalinda wake zao.
Pia inatoa wito kwa viongozi wa dini kujenga uelewa kwa jamii, hasa kwa
wanaume juu ya wajibu wao wa kusimamia haki, usawa na amani katika familia
zao.
Kwa mujibu wa rikodi za TAMWA ZNZ, tokea mwaka 2016, matukio 27 ya
mauwaji ya wanawake na watoto yameripotiwa (wanawake 22 na watoto
watano) na matukio zaidi ya 15 ya vipigo kwa wanawake tokea mwaka 2021,
ambapo ni matukio machache yaliyopatiwa hatia za sheria.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
TAMWA ZNZ calls for those involved in the incident of violence against
the woman be punished
PRESS RELEASE
TAMWA ZNZ calls for those involved in the incident of violence against
the woman be punished
The Tanzania Media Women’s Association, Zanzibar (TAMWA ZNZ) is
deeply saddened by a recent incident in Unguja, where Khadija Shaaban Ali
(34) allegedly attacked and injured her co-wife, Maimuna Said Suleiman (38),
with a knife, causing her severe pain and serious injuries.
According to media r
eports, including ZBC Radio’s Habari za Mawio program aired on February
11th 2025, the victim, Maimuna Said Suleiman (38), was allegedly attacked by
her co-wife, Khadija Shaaban Ali (34). The assault reportedly took place after
the two women were driven home together by their husband to the second
wife’s residence in Chukwani, West Urban District.
According to Mawio, the husband entered the house, leaving his two wives
alone and it was from that point the incident began. Reports indicate that
Maimuna was attacked with knives and screamed for help, but even her husband
failed to respond in time.
TAMWA ZNZ is saddened by the incident in which Khadija attacked her co-
wife, causing her severe physical harm.
Furthermore, TAMWA ZNZ is particularly concerned about the husband’s
action, as he left his wives alone without any precaution, despite being aware of
their relationship and emotions.
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tzTAMWA ZNZ emphasizes that strict legal measures should be taken against all
involved in this incident to serve as a lesson and prevent individuals from taking
the law into their hands.
TAMWA ZNZ urges the government to assess the capability of men who marry
more than one wife, ensuring they have the means to provide for and protect
their wives.
Additionally, TAMWA ZNZ calls on religious leaders to educate communities,
especially men, about their responsibility to justice, equality, and peace within
their families.
According to TAMWA ZNZ records, since 2016, 27 incidents of women and
child murders have been reported (22 women and 5 children), along with more
than 15 incidents of severe domestic violence against women since 2021, where
only a few of these incidents have reached legal remedies.
Dkt. Mzuri Issa,
Mkurugenzi,
TAMWA ZNZ.
@TAMWA_Zanzibar
www.tamwaznz.or.tz