
Vyombo vya habari kuandika habari zinazohusu mwanamke kiongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania – Zanzibar TAMWA ZNZ inaviomba vyombo vya habari kuandika habari za wanawake na uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kwa lengo la kutoa uelewa kwa jamii.
Katika muktadha wa mabadiliko ya tabianchi, vyombo vya habari vinachukuwa jukumu muhimu katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu athari za tabianchi, mbinu za kukabiliana nazo, na umuhimu wa uhifadhi wa mazingira. Kupitia vyombo vya habari, jamii inapata taarifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, mbinu za kilimo kinachohimili ukame, na njia za kupunguza uchafuzi wamazingira.
Pamoja na taarifa muhimu zinazohusu mabadiliko ya tabianchi kutolewa kupitia vyombo vya habari lakini tafiti za hapa Zanzibar zinaonyesha kwamba sauti za wanawake hazipewi nafasi ipasavyo katika vyombo vya habari.
Utafiti uliofanywa na TAMWA ZNZ mwaka 2024 ulionyesha kwamba jumla ya vipindi 2600 viliandaliwa na kurushwa hewani na ZBC na Assalam Radio ambapo kati ya hivyo 11 pekee ndivyo vilivyohusu mabadiliko ya tabianchi ambayo ni sawa na asilimia (0.9%).
TAMWA ZNZ inatambua mchango mkubwa wa wanahabari katika kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi kwa wakati. Vyombo vya habari vimeendelea kuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii kuhusu haki za wanawake na watoto, usawa wa kijinsia, ushiriki wawanawake katika uongozi, na kujenga uelewa katika kukabiliana na vitendo vya
udhalilishaji wa kijinsia.
Kwa ushirikiano wa karibu na vyombo vya habari, TAMWA ZNZ imefanikiwa kutoa jumlaya habari 778 kwa mwaka 2024 kupitia programu mbalimbali na vyombo tofauti vya habari.
Kati ya hizo, habari 502, zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, 120 kwenye magazeti, 101 kwenye redio, na 55 kwenye televisheni.
Kwa upande wa program inayohusu mwanamke kiongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, (ZanzAdapt) pekee kuanzia Novemba, 2024 hadi February 2025 imechapichwa habari, vipindi na Makala, Radio 53 sawa na asilimia 45.7%, Magazeti 22, sawa na asilimia 19%, Social media 32, sawa na asilimia 27.6% na TV ni 9 sawa na asilimia 7.9%.
TAMWA ZNZ inatoa pongezi za dhati kwa vyombo vya habari na inaomba kuzidi kushirikiana kwa kutoa taarifa mbali mbali zinazohusu mabadiliko ya tabianchi kwa lengo la kuinusu jamii.
MWISHO
———————————————————————————————————————————————————————————————————-
PRESS STATEMENT
Media Coverage on Women Leaders in Addressing Climate Change
The Tanzania Media Women’s Association – Zanzibar (TAMWA ZNZ) urges media outlets to highlight the role of women in leadership in addressing climate change, aiming to raise awareness within society.
In the context of climate change, the media plays a crucial role in educating communities about its impacts, adaptation strategies, and the importance of environmental conservation. Through the media, people receive information on changing weather patterns, climate-resilient farming techniques, and ways to reduce environmental pollution.
Despite the availability of vital information on climate change, studies conducted in Zanzibar reveal that women’s voices are not adequately represented in media coverage.
A study conducted by TAMWA ZNZ in 2024 found that out of 2,600 programs aired by ZBC and Assalam Radio, only 11 addressed climate change, representing a mere 0.9%.
TAMWA ZNZ recognizes the significant contribution of journalists in ensuring that society receives timely and accurate information. The media has consistently played a leading role in educating the public on women’s and children’s rights, gender equality, women’s participation in leadership, and raising awareness on combating gender-based violence.
Through close collaboration with the media, TAMWA ZNZ successfully disseminated a total of 778 news pieces in 2024 through various programs and media platforms. Among these, 502 were published on social media, 120 in newspapers, 101 on radio, and 55 on television.
Regarding the program focused on women leaders in addressing climate change (ZanzAdapt), from November 2024 to February 2025, a total of 53 radio programs were aired, accounting for 45.7%, 22 newspaper articles (19%), 32 social media posts (27.6%), and 9 television features (7.9%).
TAMWA ZNZ spreads its sincere appreciation to the media and calls for continued collaboration in disseminating information on climate change to support and protect communities.
END