About Us

TAMWA is a national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987. TAMWA Zanzibar became fully self-governing and operational in both Isles of Unguja and Pemba since 2004. In January 2007, it attained its own separate registration.

Contact Info

Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari za Takwimu zaWanawake na Uongozi Kufanyika Mei 2, 2026.

30/04/2026
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari za Takwimu za
Wanawake na Uongozi Kufanyika Mei 2, 2026.
Tuzo za Umahiri za Waandishi wa Habari za Takwimu za Wanawake na Uongozi
zinatarajiwa kufikia kilele chake siku ya Jumamosi, tarehe 2 Mei 2026, kupitia hafla ya
utoaji wa tuzo itakayofanyika kuanzia saa 2:00 usiku katika Ukumbi wa Madinatul Bahr
Hotel, Mbweni, Zanzibar.
Hafla hiyo inaandaliwa kwa ushirikiano kati ya Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu
Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Jumuiya ya
Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO), Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar (WEMA) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar
(TAMWA-ZNZ).
Mgeni Rasmi katika tuzo hizi anatarajiwa kuwa,Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na
Michezo Dkt. Riziki Pembe Juma.
Huu ni msimu wa tano kufanyika kwa tuzo hizi ambazo zina lengo la kutambua na
kuthamini kazi za waandishi wa habari wa Zanzibar wanaoandaa na kusambaza habari
ya kina yanayoangazia mafanikio, changamoto na mchango wa wanawake katika nafasi
za uongozi.Aidha, kwa mwaka huu tuzo hizi zimeongeza vipengele vipya vya watengenezaji maudhui
na wahamasishaji wa jamii ili kutambua pia juhudi zao katika kusaidia kukuza usawa wa
kijinsia na nafasi za uongozi kwa wanawake.
Hafla hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki wapatao 150, wakiwemo waandishi wa
habari, wahariri, wamiliki wa vyombo vya habari, wawakilishi wa asasi za kiraia, taasisi
za serikali kutoka Unguja, Pemba na Dar es Salaam, pamoja na wadau mbalimbali wa
maendeleo na itaoneshwa mubashara kupitia YouTube ya TAMWA ZNZ, ZBC TV pamoja
na MSHINDO TV ili kuwezesha wananchi wengi kufuatilia tukio hili muhimu.
Kwa mwaka huu, jumla ya kazi 252 zimewasilishwa ikiwemo vipindi vya redio, makala za
magazeti, pamoja na maudhui ya mitandao ya kijamii. Kazi hizi ziliandaliwa na kurushwa
kati ya Januari hadi Disemba 31, 2025.
Kupitia tuzo hizi, tunaendelea kudhihirisha dhamira ya dhati ya kuimarisha nafasi za
wanawake katika uongozi, kukuza usawa wa kijinsia na kuhimiza matumizi ya uandishi
wa habari wa takwimu kama nyenzo muhimu ya kuleta mabadiliko ya kijamii na
maendeleo ya taifa.
Tuzo hizi zinafanyika ikiwa ni utekelezaji wa programu ya Kuimarisha Nafasi za Uongozi
kwa Wanawake (SWIL) inayotekelezwa na JUWAUZA, ZAFELA, PEGAO na TAMWA ZNZ
kwa kushirikiana na Ubalozi wa Norway nchini Tanzania.
MWISHO.

Subscribe to our
News and Presses

***We Promise, no spam!

A national level Non-Governmental Organization known as Tanzania Media Women’s Association formed in 1987.The registration number is 493 under Zanzibar Society Act No. 6 of 1995

We’re Available

Monday : 08.00 - 10.00
Tuesday : 08.00 - 10.00
Wednesday : 08.00 - 10.00
Thursday : 08.00 - 10.00
Friday : 09.00 - 07.00
Saturday : 10.00 - 05.00
Sunday : 10.00 - 05.00